WANACHAMA WA CUF WAANZA KURUDISHA KADI KWA HAMAD

Mbunge wa Jimbo la Wawi, Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akionesha baadhi ya kadi alizodai zimekuwa zikirudishwa na baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono kutokana na hatua zake alizozichukua na pia kutokana na kufukuzwa kwenye Chama. (PICHA NA KASSIM MBAROUK)
Mbunge wa Jimbo la Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu kufukuzwa kwao kwenye Chama cha Wananchi (CUF) na hatua wanazozichukua katika suala hilo. Kulia ni mmoja wa wanachama aliofukuzwa nao, Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Doyo Hassan.
Mbunge wa Jimbo la Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akionesha kitabu alichokiandika, kutokana na kile alichodai kuwa ni baadhi ya mambo yaliyokuwa yakikirudisha nyuma Chama chao cha CUF, ambacho baadaye alishutumiwa na uongozi wa juu wa chama chake kwa kukitoa na kukisambaza kwa wanachama. Kulia ni mmoja wa wanachama aliofukuzwa nao, Doyo Hassan.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuelezea maamuzi yaliyochukuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho dhidi ya wanachama 14, waliokiuka miiko ya uongozi na uanachama ndani ya chama. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa CUF, Ally Seif.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA