Watu 40 watoweka katika ajali ya meli


Wakuu wa forodha wa Utaliana wanasema watu kama 40 bado wametoweka, baada ya meli ya abiria iliyobeba watu zaidi ya 4000 kwenda mrama katika mwambao wa Utaliana.
Meli ilizama Utaliana

Shughuli za uokozi zimeendelea kutwa, huku wazamia mbizi wakipekua upande uliozama wa meli hiyo, Costa Concordia.

Msemaji wa walinzi wa pwani alieleza inawezekana kuwa watu wengine bado wako ndani ya meli.

Abiria wawili kutoka Ufaransa na baharia mmoja kutoka Peru wanajulikana kuwa wamekufa.

Mkuu wa kampuni inayomiliki meli hiyo, Gianni Onorato, alisema ushahidi wa awali unaonesha kuwa meli iligonga mwamba;
nahodha haraka akafuata utaratibu wa kuwatoa abiria melini.

Lakini operesheni ilizuwilika kwa sababu meli yenyewe haraka ilipindukia ubavuni na kuzusha mtafaruku.

Taarifa za karibuni zinaeleza kuwa ofisi ya mashtaka ilimzuwia nahodha baada ya kumhoji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA