WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA REGIA MTEMA DAR

Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Regia Mtema (CHADEMA), wakipeleka kwenye gari baada ya kuagwa kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam leo. Amesafirishwa kwenda kwao Ifakara, Morogoro kwa mazishi.

 Askari wa Bunge wakiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Regia kwenye gari tayari kwa safari
Mbowe na Mnyika wakiangalia kwa huzuni

 Mbowe na Mnyika wakiwa na huzuni wakati jeneza lenye mwili wa marehemu Regia ukiingizwa kwenye gari
Wafuasi wa Chadema, wakiwaaga wenzao waliokuwa wakisafiri kwenda kwenye mazishi huku wakionesha alama ya vidole ya chama hicho

Wanaosafiri nao wakipungia kichadema

Sehemu ya umati wa wananchi ukisubiri kuaga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa (kulia0 akimfariji pacha wa marehemu Regia

Mama mdogo wa marehemu Regia Mtema, Benadeta Mtema (wa pili kushoto0 akilia kwa uchungu. Mama huyo ni mmoja wa watu waliojeruhiwa katika ajali iliyomuua Regia. Kulia na Babab Mzazi wa Regia. Estalatus Mtema.

Msafara ukiondoka Karimjee kuele4ka Ifakara, Moro, kwa mazishi.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

 Spika mstaafu Samuel Sitta, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Regia
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (katikati), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, Regia Mtema.

Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na Bob Makani wakitoa heshima za mwisho

Waziri wa Utalii, Ezekiel Maige na Mbunge wa Bumburi, Januari Makamba wakitoa heshima za mwisho

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia akimfariji pacha wa marehemu Regia Mtema
Heshima zikiendelea kutolewa kwa mwili wa Regia

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akimfariji Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi akimfariji Freeman Mbowe

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA), akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto.

Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kushoto) na Profesa Mwesiga Baregu wa CHADEMA.

Vijana wa Mtandao wa Jamii Forum wakiwa wamevalia rasmi waliposhiriki kuuaga mwaili wa aliyekuwa mwanachama wa mtandao huo, marehemu, Regia Mtema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA