Huduma za internet kero Afrika mashariki

Huduma za mawasiliano kupitia internet zimekatizwa katika ukanda wa Afrika mashariki baada ya mkondo wa mawasiliano ulioko mombasa kukatika.

Wahandisi wanasema mkongo huo uliharibiwa na meli ilioshusha nanga yake katika eneo ambalo hairuhusiwi.

Kutokana na kisa hicho kampuni za kutoa huduma za mawasiliano ya internet zimekuwa zikitoa huduma hiyo kwa viwango vya kasi ndogo kuliko inavyohitajika.

Joel Tanui, msemaji wa kampuni ya The East African Marine Systems (Teams), amesma majaribio yao yanaonyesha kuwa mkongo huo unaounganisha ukanda huu na dunia nzima umekatika kabisa.

Bw Tanui ameelezea kuwa kutokana na hilo huduma za mawasiliano kutumia internet zimeathirika nchini Kenya, Uganda, Tanzania, rwanda, Burundi, ethiopia and Sudan kusini. Huduma hizo ingawa zinapatikana kwa sasa sio kwa kasi inayohitajika.

Mkongo mwengine wa mawasiliano unaomilikiwa na kampuni ya East African Submarine cable systems (EASSy) ambao unaunganisha nchi zilizoko kusini na kaskazini mwa Afrika na dunia nzima pia nao ulikatwa na meli hiyo.

Uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo ambapo meli iliruhusiwa kushusha nanga yake katika eneo ambalo hairuhusiwi.

Kazi ya kurekebisha mkongo huo itachukua muda wa wiki mbili, kulingana na msemaji wa Kampuni ya TEAMS.

Kisa hicho kimeathiri sana shughuli na biashara zinazotegemea sana huduma ya mtandao wa internet kote mjini Nairobi. Hasaa Kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi ambazo zimekuwa zikichuma kupitia huduma ya internet tangu mkongo huo wa mawasiliano uzinduliwe.

Mkongo huo wa mawasiliano ulizinduliwa mwaka wa 2009 ukiwa ni ubia kati ya serikali ya Kenya na idara ya mawasiliano za miliki za Emirati.

Huduma hiyo ilipunguza gharama za internet maradufu kwani kabla ya hapo kampuni nyingi zilitegemea satelite kutoa huduma hiyo, njia ambayo ni ghali mno.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI