Kesi ya ubaguzi kumuandama Rais Zuma

Chama cha Democratic alliance kinasema kuwa uamuzi wa mwendesha mashataka wakati huo wa kuondoa mashataka dhidi ya Rais Jacob Zuma ulichukuliwa kwa misingi ya kisiasa na sio kisheria.
Anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na ulanguzi

Katika kipindi hicho chama cha ANC kilishuhudia mvutano mkali wa kisiasa na kulikuwa na madai kuwa idara za serikali zilikuwa zinatumiwa kuwa nyamazisha mahasimu wa kisiasa waliokuwa wanang'ang'ania madaraka.

Kanda za mazunguzmo hayo kati yao zilitumika mahakamani kama ushahidi wa njama hiyo.

Mwaka wa 2007, Jacob Zuma alifunguliwa mashataka ya kuhusika na rushwa, udanganyifu na ulanguzi.

Kesi hiyo dhidi yake iliwasilishwa siku nane baada ya kumshinda aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki kwenye mvutano wa kukiongoza chama cha ANC.

Mashtaka hayo yaliibuka baada ya aliyekuwa mshauri wa masuala ya kiuchumi wa Zuma, Shabir Shaik alipopatikana na hatia ya ulanguzi.

Mshataka dhidi ya Zuma yaliondolewa, wiki mbili kabla uchaguzi wa April mwaka 2009. Hatua hiyo iliwaudhi viongozi wa upinzani na baadhi ya mashirika ya kijamii huko Afrika kusini.

Wakosoaji wanasema lazima mahakama iamue ikiwa kweli kiongozi huyo alikuwa na hatia. Kwa hivyo uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kesi hii unasubiriwa kwa hamu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.