KIONGOZI WA AL QAEDA AKAMATWA MISRI

Maofisa wa usalama nchini Misri wanasema wamemkamata mmoja wa wakuu wa mtandao wa al-Qaeda kwenye uwanja wa ndege wa Cairo, Saif al-Adel. (PICHANI)

Saif al Adel
Alikamatwa pindi alipowasili kwenye ndege kutoka Pakistan.
Maofisa hao waliwambia wandishi habari kua walifahamu kuhusu nia yake ya kujisalimisha, na kwamba jina lake halisi ni Mohammed Ibrahim Makkawi na alikua kwenye orodha ya abiria waliosafiria ndege hio.
Mtu huyo ambaye zamani alikua nwanajeshi wa Misri akiwa wa ngazi ya kanali. Wakati mmoja alikua mkuu wa usalama wa Osama Bin Laden na pia anatakikana na Marekani kuhusianiana na mashambulio ya balozi za Marekani huko Afrika mashariki mnamo mwaka 1998.
Halikadhalika anatuhumiwa kwa kuwapa mafunzo wapiganaji wa Kisomali walioshiriki mauwaji ya wanajeshi wa Marekani 18 mjini Mogadishu mwaka 1993 pamoja na washambuliaji walioshiriki shambulio kabambe la Marekani mwezi septemba mwaka 2001.
Saif al-Adel yuko msitari wa mbele kwenye orodha ya shirika la kijasusi la Marekani FBI ambapo Marekani imetoa zawadi ya dola milioni 5 za Kimarekani kwa habari yoyote itakayowawezesha kumkamata au hata kumuua.
Maofisa wa usalama wamliambia shirika la habari la Misri, Mena kua Saif Adel alizuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Cairo alipowasili leo jumatano baada ya safari yake kutoka Pakistan akipitia Dubai.
Kamanda huyu wa vikosi vya Misri ambaye alihudumu katika vikosi maalum, ana umri ulio kati ya miaka 50 hivi na alikwenda kushiriki vita nchini Afghanistan mwaka 1980 akijiunga na kundi la Mujahidin dhidi ya vikosi vya Urussi.
Tangu mwaka 1987 amekua akisakwa na wakuu wa Misri alipotuhumiwa kwa kutaka kuunda tawi la kijeshi la kundi la Al Jihad nchini Misri kwa nia ya kuiondoa madarakani serikali ya Misri.
Baadaye Saif al-Adel alijiunga na al-Qaeda na moja kwa moja kua mkuu wa usalama wa Osama Bin Laden. Aliridhi majukumu mengi yaliyokua yakishikiliwa na Kamanda wa jeshi Mohammed Atef alipofariki kufuatia shambulio la Wamarekani mwezi novemba mwaka 2001.
Baada ya uvamizi wa Marekani wa Afghanistan mwaka 2001, inaaminika kua Saif al-Adel alikimbilia nchini Iran pamoja na Saad Bin Laden, mwanawe kiongozi wa al-Qaeda leader marehemu Osama Bin Laden.
Nchini Iran inasemekana kua walizuiliwa na wakuu wa serikali ya mapinduzi ya Iran ingawa wakuu hao walikanusha habari za kuwemo nchini mwao.
Zimekuepo tetesi kua Saif aliteuliwa kama kiongozi wa mda wa al-Qaeda baada ya kifo cha Osama Bin Laden mwezi May mwaka jana katika mji wa Abbottabad huko magharibi mwa Pakistani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.