Makamu wa Rais wa Uchina, Xi Jinping, ambaye anatarajiwa kuwa kiongozi wa juu wa nchi baadaye mwaka huu, amewasili nchini Marekani akiwa katika ziara rasmi.
Anatarajiwa kukutana na Rais Barack Obama katika Ikulu ya nchi hiyo baadaye leo, kujadiliana masuala mbalimbali yenye msuguano kati ya nchi mbili hizo.
Miongoni mwa masuala hayo ni mvutano kuhusu Syria, Iran na Korea Kaskazini, uimarishaji wa majeshi katika Asia Mashariki na nakisi kubwa ya kibiashara ya Marekani na Uchina.
Bwana Xi anaonekana kuwa ndiye atakayechukua uongozi wa Chama cha Kikomunisti katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika Beijing mwishoni mwa mwaka huu.
Comments