Mtoto Cesilia Edward afariki Dunia

Mtoto Cesilia Edward amefariki dunia saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwaajili ya matibabu

Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.

Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi mimi na Tanzania ilifanikiwa kumpeleka marehem Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.

Cesilia alikuwa mtoto ya tima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagara kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyo nayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alio nao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.

Marehemu alifikishwa hospitali jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauli ulipo mkuta Mungua ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi Amen.CHANZO;FULLSHANGWE BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.