MWEKEZAJI KAPUNGA MBARALI MBEYA AFIKISHWA MAHAKAMANI


SERIKALI imemfikisha mahakamani Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kampuni ya Expotr Trading Group amefikishwa mahakama ya wilaya ya Mbeya kwa makosa mawili tofauti likiwemo kosa la kula njama la kutenda kosa la kuharibu mali na kuharibu mali za wananchi kwa hila.

Mwekezaji huyo alifikishwa mahakamani hapo jana kwa makosa hayo aliyoyatenda Januari 12 hadi 14, mwaka huu kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa ambapo alimwaga sumu katika mashamba ya wakulima zaidi ya 154 wa Kijiji cha Kapunga wilayani humo.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Seif Kulita, Mwendesha mashitaka wa Serikali Griffin Mwakapeje alisema kuwa washitakiwa hao aiwemo Meneja wa shamba hilo Walder Vermaak, Afisa ugani Serger Bekker na Rubani wa ndege Andries Daffe walitenda kosa hilo wilayani humo na kuharibu mazao ya wakulima hekari 489.5.

Mwakapeje alisema kuwa wawekezaji hao wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 226 (i) cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002 la kuharibu mazao hayo ya Mpunga wa wakulima wanaolima eneo linalojulikana kwa jina la Mpunga moja.

Baada ya mashitaka hayo, Hakimu Kulita alpowauliza washitakiwa hao wote kwa pamoja walikana shitaka hilo ambapo wakili anaowatetea watuhumiwa hao Ladislaus Rwekaza aliomba dhamana kwa wateja wake na hatimaye mahakama ikaridhia kwa Masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja mweye mali isiyohamishika isiyopungua Shilingi Milioni kumi.

Aidha Hakimu huyo alitoa sharti kwa watumumiwa hao kuwa mbali na sharti la kuwa na mdhamini mmoja na mali isiyohamishika pia watuhumiwa waliytakiwa kukabidhi hati za kusafiria na kwamba hawapaswi kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya na kama watahitaji kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya ni lazma wapate kibali cha mahakama hiyo ambapo washitakiwa walitimiza masharti hayo.

Baada ya Masharti hayo watuhumiwa walidhaminiwa na Uwesu Msumi mkazi wa Jijini Dar Es Salaam na kukabidhi hati ya nyumba yenye namba 229 Block J iliyopo Mbezi Jijini Dar es Salaam, Christian Basil Mmas aliyekabidhi hati ya nyumba yenye namba 109 iliyopo Geza Ulole Jijini Dar es Salaam na Sunnil aliyetoa hati namba 254 iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kesi hiyo itatajwa tena Machi 6, mwaka huu.


Baadhi ya wananchi walioathiriwa na sumu hiyo wakati ndege ikimwaga mashambani na kushuhudiwa ni pamoja na Michael Shija, Severina Mbwilo, Elikana Nsemwa, Edward Simkoko, Gaidon Peter Ngogo (54), Jailo Esau (22), Jackson Mwandemange (52), Catherina Shipela (50), Edda Ngosha (35), Julius Isega(50), Ramadhan Nyoni (52)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.