NHIF KUKUTANA NA WADAU NCHI NZIMA
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia wiki ijayo unatarajia kufanya mikutano ya wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini ambapo utaanza na Mkoa wa Lindi na Mbeya.
Mikutano hiyo itawashirikisha wadau wa kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa kiserikali, viongozi wa kisiasa, viongozi wa kidini, watoa huduma na wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Akizungumzia ratiba ya mikutano hiyo Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Eugen Mikongoti amesema mikutano hiyo itaanzia katika mikoa ya Lindi na Mbeya Februali 28, Mwaka huu na itaendelea hadi mwezi April katika mikoa yote nchini.
Amesema lengo la mikutano hiyo ni kuwakutanisha watendaji wa NHIF na CHF pamoja na wadau wake ili kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za Mfuko tangu kuanzishwa kwake lakini pia kuwasilikiza wadau wake hasa katika mambo mbalimbali wanayokutana nayo wakati wa kupata huduma za Mfuko.
Aidha Bw. Mikongoti amesema mikutano hiyo itatoa fursa kwa wadau kujadiliana kuhusu maendeleo ya kiutendaji na changamoto zinazoukabili Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha huduma zake.
Ameongeza kuwa mikutano hiyo ni utaratibu uliowekwa na NHIF ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya ushirikishaji wa wadau katika shughuli zake za kila siku na hasa kukutana nao katika maeneo yao.
“Tunaamini kuwa tutatakopokamilisha mikutano hii hapo mwezi Aprili mwaka huu, tutakuwa tumekusanya maoni wa wadau wa kada mbalimbali ambayo yatatusaidia kuendeleza mafanikio tuliyoyapata katika kipindi hiki cha miaka kumi ya uhai wetu na kupambana na changamoto zinazotukabili kwa sasa”, alisema Bw. Mikongoti.
Bwana Mikongoti amewaomba wadau walioalikwa kushiriki katika mikutano hiyo kuwa wawazi na kutoa maoni yao kwa lengo la uboreshaji.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekuwa na taratibu mbalimbali za kukutana na wadau wao ikiwa ni pamoja na mikutano ya kila mwaka ya Wahariri na Waandishi wa habari Waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, mikutano ambayo imekuwa na mrejesho mzuri na kusaidia kuboresha mambo mbalimbali katika utoaji wa huduma kwa wanachama.
Ciooo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI