TIGO YAZIDI KUWAMWAGIA WASHINDI MAMILIONI,LAPTOP

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro (kushoto) akimkabidhi Anitha Kasanga mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 4, baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa promosheni ya 'Zamu Yako Kushinda' Dar es Salaam leo. Katikati ni Mratibu wa Matukio wa Tigo, Edward Shila.
Anitha akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, jinsi fedha hizo atakavyozitumia ambapo alisema kiasi atakitumia kupata masomo zaidi
Mkazi wa Makongo Juu, Fidelis Simon Mosha akikabidhiwa hundi yenye thamani ya sh. milioni 4 baada ya kuwa miongoni mwa washindi 19
Mama Mkazi wa Mbezi Luis, Hellen Jumbe(65), akikabidhiwa zawadi ya kompyuta ndogo aina ya Samsung. Alikuwa miongoni mwa washindi 38 waliozawadiwa laptop.
Mkazi wa Ubungo, Dar, Priscus Tarimo (kulia) akizawadiwa laptop

Tigo yawazawadia washindi wa mwisho wa promosheni ya “ZAMU YAKO KUSHINDA”

28 Februari, 2012, Dar es Salaam. Katika kumalizia promosheni ya “Zamu Yako Kushinda,” kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi kumi na tisa, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi wa kwanza na washindi wengine 38 wamezawadiwa Laptop aina ya Samsung ikiwa ni zawadi ya washindi wa pili na wa tatu. Jumla ya milioni 328 za kitanzania zimetumika kuwalipa washindi waliopatikana katika kipindi cha siku 82 za promosheni iliyoanza kuanzia tarehe 30 Novemba, 2011 hadi tarehe 19 Februari, 2012.

Baadhi ya washindi wa milioni nne kutoka mikoa mbalimbali ni: Fidelis Simon (Dar); Magreth Masasi (Singida); Neema Ngowi (Morogoro) na Edwin Felix (Dodoma).

Baadhi ya washindi wa Laptop aina ya Samsung kutoka mikoa mbalimbali ni : Gatuki Gatuki (Dar); Beatrice Kalaghe (Tanga); Bernard Silozi (Tabora); Mahmoud Seif (Lindi) na Hellen Jumbe (Dar).

“Tungependa tuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii, pia tungependa kuwapongeza washindi wote” alisema Alice Maro, Afisa Mahusiano wa Tigo. “Tungependa pia kuwakumbusha wateja wetu kuwa wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni yetu mpya ya Kupiga simu za kimataifa, ambapo mshindi mmoja mwenye bahati atajishindia safari iliyolipiwa kwenda mahali alipopiga simu zaidi,” alisema.

Kushiriki katika promosheni hii mpya, wateja wanatakiwa kutumia zaidi ya shilingi 1,000 kupiga simu za kimataifa. Jinsi watakavyopiga simu za kimataifa zaidi kwa kutumia Tigo ndivyo watakavyojiongezea nafasi ya kushinda.

Washiriki lazima wawe na miaka kumi na nane na kuendelea ili kuweza kushiriki kwenye promosheni hii. Shindano hili ni kwa ajili ya raia wa Tanzania ambao ni wateja wa Tigo. Promosheni hii imeanza tarehe 22,Februari hadi Aprili 22, 2012.


Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA