Uhusiano:Ufanye nini kurudiana naye?





“NAMPENDA sana, lakini nashindwa cha kufanya juu yake. Natamani arudi tena katika mikono yangu, nimejaribu kila njia imeshindikana,” ndivyo baadhi ya watu wanavyojisemea.
Yawezekana wewe ni kati ya watu ambao wenzi wao wameachana nao, sasa wanatamani kuwarudia lakini hawajui la kufanya.
Pole sana, lakini kitu cha kwanza cha kuangalia ni kama mwenzi ambaye mmeachana anaye mtu au la. Na kama anaye mtu, je mtu huyo tayari anafahamika kisheria, au la.
Ikiwa hajulikani, hilo laweza kuwa ni jambo la kushukuru. Lakini kama hana mtu kabisa, hilo laweza kuwa jambo zuri zaidi kwako. Cha msingi ni kutuliza akili na kujivuta karibu nae kwa staili mbalimbali.
Kuharibika kwa uhusiano wa mapenzi, si jambo lenye kufurahisha hata kidogo. Yaweza kuwa ni jambo lisilowafurahisha wote au mmoja wao. Kama inawezekana ni vizuri kuendelea na uhusiano na mtu ambaye unamfahamu, kuliko kuanzisha uhusiano na mtu mpya.
Kuna msemo kwamba heri shetani unayemjua kuliko malaika usiyemfahamu….kwamba wakati mwingine watu ambao tuko nao kwa muda mrefu, huwa tunawaona hawana maana, badala yake tunafikiria kuwa na watu wapya.
Wengine huwa wanashindwa kukumbuka kwamba hata hao ambao tuko nao, wakati tunaanzisha uhusiano walikuwa watamu kuliko. Wanashindwa kupata muda wa kutafakari, sasa hakuna tena raha, badala yake ni shida au kuna mambo yasiyo mazri yanatoendelea baina yao. Kwanini hakuna raha katika uhusiano huu, wakati zamani kulikuwa na raha?
Wengi hukimbilia kuanzisha uhusiano na watu wapya, badala ya kukaa chini na kutafakari kwanini uhusiano nilionao sasa si mzuri au una mikwaruzo.Wengi hukimbilia kusema aaah bora kuanzisha uhusiano na mtu mwingine, jambo ambalo sio sahihi.
Ikiwa kazi yako ni kuacha na kusaka wengine kwa sababu huyu hafai, amini ninakwambia utaacha wengi. Ni vizuri kutafakari kwa umakini mkubwa kwamba matatizo katika maisha ya uhusiano yapo, kwa maana hiyo unapaswa kufanya kila uwezalo kuhakikisha uhusiano wako unakuwa mzuri.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, kuachana si jambo linalofaa. Ni muhimu kuangalia namna ya kufanya ili kuendeleza uhusiano na mtu ambaye unaye. Kama ambavyo mkulima anapokuwa na shamba, labda amepanda mahindi, na magugu yakaota, anachokifanya huwa ni kutafuta dawa ya kuua magugu yaliyoota, ili mahindi yake yaweze kukua vizuri.
Kwanini wewe kunapokuwa na migogoro, wazo lako la kwanza ni kuchana? Yuko wapi ambaye utakuwa nae hatakukwaza? Ni ngumu, ikiwa hata wazazi ambao tumetoka matumboni mwao, kuna wakati tunakwaruzana nao, iwe watu ambao tumekutana nao tu mitaani?
UFANYE NINI IKIWA BADO UNAMPENDA? Kuna njia nyingi za kufanya kurudiana na mtu ambaye mmeachana nae.
1. Usiongee sana: Ikiwa mmekutana nae labda njiani nk, usizungumze nae sana, wala usiongee sana mambo ya zamani. Kwa mfano unaweza kumsalimia na kumwambia nina kazi kidogo tutaonana. Tabia ya aina hii itamwonyesha huyo mtu ambaye mmeachana kwamba ‘huna njaa nae sana’…jambo la namna hii huwa linawauza sana wanawake.
2. Ongea jambo lolote la kumchekesha; Jambo mnaweza kukutana kwa bahati mbaya, tumia muda huo mfupi kuzungumza vitu vya kufurahishana. Kitendo cha kumfanya mwenzi wako mliyeachana kucheka, kinawasogeza karibu. Hata mnapoachana, ataendelea kukufikiria.

3. Usionyeshe kuumia unapomwona ana ukaribu na mtu wa jinsia yako; Kuna wengine hukunja ngumi au hata kufikiria kufanya lolote baya, kisa kamwona mwenzi wake yuko karibu na mtu mwingine. Onyesha ukomavu, wala usibabaishwe na jambo lolote.

Unapoona yuko na mwingine, nawe labda unaendelea na mambo yako au uko na shughuli zako, endelea kufanya hivyo, wala usionyeshe kuumia.
4. Usiongee sana kwenye simu; Ni jambo la msingi kuhakikisha hata kama unapata nafasi ya kuongea nae kwenye simu, usiongee sana, wala usipende sana kuzungumzia mambo ya zamani. Fanya kama vile ndio kwanza mnaanza uhusiano, wakati mwingine mjulie hali nk.
5. Uwe wa kwanza kumuaga, baada ya kuwa mmekutana; Ikiwa mmekutana kwa bahati mbaya au nzuri, ni vizuri kuhakikisha unakuwa wa kwanza kumuaga.
Wapo wengine husema kuwa ni vizuri kuwa karibu na mtu wa jinsia nyingine halafu jipeleke karibu na huyo mliyeachana. Hiyo siyo sahihi, badala yake hata kama alikuwa anafikiria kuwa nae, mawazo hayo yanakufa kabisa.
Ni vizuri kuonekana ni mwenye kufaa kwa mwenzi wako wa zamani, sio kuendekeza tabia kama hizi za kuwa na mwanamke au mwanaume mwingine, eti kwa kuamini ataona shauku ya kuwa nawe.

Dismas Lyassa ni mtaalam wa uhusiano aliyesajiliwa na serikali kupitia kituo cha ushauri, Global Source Watch, kwa msaada zaidi piga 0653777700/0755444555.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.