ADHABU ZILIZOTOLEWA NA TFF KWA YANGA ZASITISHWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU RUFANI YA KLABU YA
YANGA
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF, kwa kutumia
mamlaka aliyopewa na Kanuni ya 129 ya Kanuni za Adhabu za FIFA, leo
tarehe 24 Machi, 2012, ameamuru kusitishwa (provisional suspension) kwa
adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wa Timu ya
Yanga ya jijini Dar es Salaam. 

Chini ya Kanuni hiyo, Mwenyekiti anayo mamlaka ya kusitisha utekelezaji wa adhabu yoyote ile pale anapoona
kwamba ukiukwaji unaolalamikiwa hautaweza kupatiwa ufumbuzi wa
haraka bila kuathiri haki za wale wanaokata rufani.

Usitishwaji wa adhabu hizo, ambao utadumu kwa muda wa siku 14,
kuanzia tarehe ya kusitishwa huko, una nia ya kutoa fursa kwa Sekretarieti
ya TFF kuwasilisha rufani ya Yanga pamoja na maelezo yanayohusiana na
rufani hiyo, mbele ya Kamati ili isikilizwe na hatimaye kuitolea maamuzi.

Kamati inasisitiza kwamba adhabu zilizotolewa na mwamuzi wa mchezo
huo katika dakika 90 za mchezo hazitahusika na amri hii ya kusitisha
utekelezaji, na wachezaji wanaohusika na adhabu hizo za mwamuzi
wataendelea kutumikia adhabu zao hadi hapo watakapomaliza au pale
maamuzi mengine yatakapotolewa.

Aidha, Kamati imeelekeza kwamba TFF ifanye juhudi za kuharakisha
usikilizwaji wa rufani hiyo ili kuwawezesha wachezaji waliohusika kujua
hatma yao kimichezo.

Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 24 Machi, 2012.
.....................................................
Comm. (rtd) Alfred Tibaigana
Mwenyekiti wa Kamati

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI