BIA YA BALIMI EXTRA LAGER YABADILI MUONEKANO WAKE.


Kutoka kulia ni Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, Meneja mauzo wa kanda, Malaki Staki, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa na  na, Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah,   wakigonganisha chupa ikiwa ni ishala ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi Extra Lager  uliofanyika Yatch Klabu mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la leo

BIA YA BALIMI EXTRA LAGER YABADILI MUONEKANO WAKE.

Mwanza 24, 2012: Kampuni ya Bia TBL kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imetambulisha rasmi muonekano mpya wa Bia hiyo maarufu katika kanda ya ziwa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa bia hii ya Balimi Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager ilianzishwa rasmi mwaka 1999 ikiwa ni tuzo maalum kwa wakazi wa kanda ya Ziwa kwa kazi nzuri wanazofanya katika sekta za Kilimo, uvuvi, madini nk. Tangu mwaka huo, bia hii imekuwa ikipendwa sana na hata kuwa bia inayoongoza kwa mauzo kuliko bia zote kwa kanda ya Ziwa. Kitu kikubwa kinachoipa bia ya Balimi mafanikio haya ni ladha yake ya kuvutia na ubora wake wa  hali ya juu.

Tangu ilipoanzishwa, bia ya Balimi Extra lager imeshafanya badiliko moja tu katika kuboresha lebo yake, na hii leo tunashuhudia mabadiliko makubwa katika muonekano wa bia yetu tuipendayo. Sasa iko katika chupa ya kisasa yenye shingo ndefu, na lebo yake imefanyiwa maboresho makubwa, yote haya ni kuhakikisha kuwa Bia ya Balimi Extra Lager inaendana na mabadiliko ya wateja wake ambao wamekuwa wakibadilika kuendana na wakati na mazingira yanayowazunguka. Kitu cha msingi tunachowahakikishia wapenzi wa bia hii ya Balimi ni kuwa kilichobadilika ni muonekano wa nje tu, ladha ya bia hii ni ileile wanayoipenda na wala haitobadilika. Kwa mabadiliko haya tuna imani kubwa kuwa bia ya Balimi sasa itapendwa zaidi na hivyo mauzo yake kuongezeka sana. Alisema bi Edith Bebwa.

Nae Meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alielezea mchango mkubwa ambao bia ya Balimi inatoa katika kanda ya ziwa kwa kuainisha maeneo mbalimbali ya udhamini akisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa karibu sana na wakazi wa kanda ya Ziwa kwa kuhakikisha inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza michezo na tamaduni za kanda yetu ya ziwa. Bia hii inadhamini mashindano maarufu ya Mitumbwi yanayofanyika kila mwaka kanda ya Ziwa. Pia inadhamini mashindano ya ngoma za asili za kanda ya ziwa na vile vile inadhamini tamasha la kudumisha utamaduni wa mkoa wa Tabora lijulikanalo kama “Tamasha la Mtemi Mirambo. Haya ni baadhi tu ya mambo mengi ambayo bia ya Balimi inafanya, hivyo tunaomba wakazi wa kanda ya ziwa waendelee kuiunga mkono bia hii ili iweze kuwafanyia mambo makubwa zaidi, maana wahenga walisema “Jivunie Kilicho Chako” Alimalizia Bw. Butallah.

Akifafanua kuhusu mabadiliko ya bei; Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kanda Bw. Malaki Sitaki alisema; Bei ya Balimi kwa chupa moja kwa mlaji haijabadilika, itaendelea kuuzwa kwa shilingi 1,700/- tu, kitakachobadilika ni bei kwa sanduku, ambapo sasa sanduku la Bia ya Balimi yenye shingo ndefu itakuwa shilingi 27,200/- tu badala ya shilingi 34,000/- ya awali. Hii inatokana na idadi ya chupa katika sanduku ambapo sasa kuna chupa 20 kwa sanduku badala ya chupa 25 za awali. Bia hii yenye muonekano mpya itaanza kupatikana katika maeneo yote kuanzia kesho tarehe 25 machi.
BALIMI EXTRA LAGER - KANDA YANGU, BIA YANGU.

--MWISHO –



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*