Kinondoni Revival kumpeleka 'Mtu wa Nne' Pasaka

KWAYA mahiri ya Kinondoni Revival inatarajia kutumbuiza katika tamasha la muziki wa Injili la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, alisema kundi hilo la kwaya limeahidi kufanya mambo makubwa.

Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa waimbaji hao wa nyimbo za kumsifu Mungu hivi sasa wanatamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, ambayo anaamini itawang'arisha katika tamasha hilo.

Msama alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Mtu wa Nne, Imekwisha, Chukua Hatua, Mtafuteni Bwana, New Season, Hakikisha, Ninakushukuru na Dini Iliyo Safi.

Pia kwaya hiyo ya Kinondoni Revival imewahi kutamba na albamu yao ya Kilio cha Mcha Mungu yenye nyimbo nane za Kilio cha Mcha Mungu, Kwanini Unataka Kujiua, Ayubu II, Vumilia Kidogo, Nafsi Yangu, Natamani Kwenda Mbinguni, Ndugu Yetu Twakutafuta na Twalilia Tanzania ambazo pia wameahidi wataziimba.

Mbali na kwaya ya Kinondoni Revival, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Rose Muhando, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kundi la Glorious Celebration.

Msama alisema baada ya waimbaji hao kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.

Ciao...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.