Maandalizi kabambe mkoa mpya wa Njombe

Mbunge wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Idundilanga. Picha zaidi tembelea :www.prince-minja.blogspot.com
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kutangaza nia ya kuugawa mkoa wa Iringa ili kuwa na mikoa miwili yaani mkoa wa Iringa na Mkoa wa Njombe, wananchi wa mkoa mpya wa Njombe hawalali hadi kieleweke. Kwa kujituma kunakostahili kuwa mfano wa kuigwa na kwa ushirikiano usiojali imani, kabila au itikadi za kisiasa wamedhamiria kuujenga mkoa wao huo kwa kiwango cha hali ya juu. Mbinu wanazotumia ni kupiga vita umaskini kwa kuchapa kazi hususan za kilimo cha mazao ya chakula (mahindi, matunda, viazi,) na biashara (miti ya mbao), kupiga vita ujinga kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya awali na msingi pamoja na kila kata kuwa na shule ya upili, na kupiga vita maradhi kwa kujenga zahanati na vituo vya afya. Wakionesha ari na msukumo mkubwa kwa Mbunge wao Mhe. Anne Semamba Makinda aliyewatembelea wananchi hao hivi karibuni, wananchi hao wanajivunia tabia yao ya kupenda kufanya kazi kwa bidii na kujituma, ardhi yenye rutuba walio nayo pamoja na ukanda wanamoishi wa nyanda za juu kusini wenye mvua za kutosha nyakati zote.
Akizungumza nao mbunge huyo aliwasisitizia kujipanga vizuri ili kuzifaidi fursa zitakazotokana na uchimbaji wa mkaa wa mawe pamoja na chuma katika migodi ya Ludewa na Liganga ambayo utekelezaji wake tayari uko katika hatua za kuanza uchimbaji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli ambazo wananchi wa Njombe wanashiriki. (Prosper Minja)
Mbunge akikagua daraja la Luponde-Kisilo la mto Hagafilo linalojengwa kwa nguvu za wananchi.
Ujenzi zahanati ya Kisilo
Pamoja na mvua kubwa wananchi wanataka kusikia Mbunge wao anawaambia nini kuhusu maendeleo yao
Baadhi ya nyumba za waalimu katika kijiji cha Ikisa.
Tatizo linalowakumba wakulima ni kutozingatiwa kwa vipimo katika mazao yao. Hii ni rumbesa ya viazi ambayo inawaumiza sana wakulima na hivyo kuiomba serikali iingilie kati.
Mwananchi akitoa maoni yake katika kitongoji cha NHC
Kituo cha Afya Idundilanga
Wananchi wa kijiji cha Mfereke.Chanzo, Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*