Eric Shigongo akiwa amembeba mtoto wa Marehemu Complex
Mmoja wa kinarihanna aitwae Babro akitetea nafasi yake
Mkoloni akikabidhi tuzo nyingine kwa Mtoto wa Marehemu Complex
Msanii wa Hip Hop Bongo, John Mkoloni (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa familia ya Vivian, huku akishuhudiwa na Shigongo.
‘Juma Nature’, (kushoto), akikabidhi tuzo kwa William Mungai mwakilishi wa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, anayeshuhudia ni Shigongo
Profesa Jay (kulia), akikabidhi tuzo kwa familia ya marehemu DJ Kim. Wanaoshuhudia ni mdogo wa DJ Kim na Shigongo.
Msanii wa Hip Hop, Joe Makini (kulia), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Father Nelly (kushoto), tukio lililoshuhudiwa na Shigongo.
DJ Choka (kulia), akikabihi tuzo hiyo kwa mwakilishi wa GWM.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd na mmiliki wa Ukumbi wa Dar Live, Eric James Shigongo, akiongea jambo  kabla ya zoezi la utoaji tuzo za wasanii wa Hip Hop kuanza
Msanii wa Hip Hop Bongo, Fid Q, akitumbuiza.
Profesa Jay Akidatisha Mashabiki
Chidi Benz Huyo
Joe Makini na G Nako wakiwa kazini.
Rihanna Mwingine akiwa kazini
Washiriki wanane waliofaulu kuendelea kwenye shindano hilo
Mmoja wa majaji wa shindano hilo, Baby Madaha (katikati), akiwanadi ‘kina Rihanna’ kwa mashabiki wamchague mmoja aendelee
Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo.
--
TAMASHA la Usiku wa Hip Hop kuamkia jana limetikisa vilivyo ndani ya kituo cha maraha cha Dar Live Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam.

Wasanii waliokuwa kwenye ‘game’ la muziki wa aina hiyo na sasa wametangulia mbele za haki walienziwa kwa kupewa tuzo mbalilmbali ambazo zilipokelewa na baadhi ya ndugu zao na marafiki wa karibu.

Wasanii walioenziwa kwa kupewa tuzo ni Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ambayo ilikabidhiwa na Juma Kassim ‘Juma Nature’ ikimsifu kwa harakati za kuifikisha Hip Hop ilipo leo, nyingine ilikwenda kwa kundi la Kwanza Unit ambayo ilikabidhiwa na Farid Kubanda ‘Fid Q’, ya DJ Kim ilikabidhiwa na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, ambapo tuzo ya Bon Love iliyokabidhiwa na Dj Tasi, marehemu Complex tuzo yake ilikabidhiwa na Mkoloni, ambapo tuzo ya GWM ilikabidhiwa na DJ Choka.

Tuzo ya Father v Nelly ilikabidhiwa na Joh Makini, ya John Mjema na Steve 2K ilikabidhiwa na G Nako, tuzo ya Saleh Jabir ilikabidhiwa na Big Willy, ya Mr Ebbo ilikabidhiwa na Fanani huku Hard Blasters wakikabidhiwa tena na Juma Nature.

Baada ya Shughuli ya utoaji tuzo, Dar Live ilizizima kwa shoo kali kutoka kwa, Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Chid Benzi. 

Mapema kabla ya zoezi hilo kuanza zilitumbuiza bendi za taarabu za Super Shine na Mashauzi Classic, huku makundi mbalimbali ya ngoma za asili na sarakasi yakitawala ardhi na anga.
Usiku huo pia kulirindima shindano la ‘Cheza, Vaa, Imba Kama Rihanna’ ambapo washiriki wawili waliyaaga mashindano hayo na kubaki washiriki wanane kati ya kumi waliokuwa wameingia kumi bora. Chanzo;Haki Ngowi Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA