MEJEA WA KITUO CHA RADIO CHA MTOTO WA LOWASSA MBARONI KWA SAKATA LA RUSHWA KURA ZA MAONI CCM ARUMERU

Zengwe la madai ya rushwa katika kumpata mgombea wa CCM, Arumeru Mashariki limeendelea kutanda kufuatia maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU)  kumkamata Meneja wa Kituo cha  Radio Five kinachomilikiwa na mtoto Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Robert Lowassa.

Kamanda wa Takukuru mkoa wa Arusha Mbengwa Kasomambuto akithibitisha, amesema Meneja huyo Jimmy Mtemu  wamemkamata akiwa ofisini kwake Njiro jijini Arusha kwa ajili ya kumhoji.

Alisema mbali na meneja huyo kukamatwa pia wanachama wengine wawili wa CCM walikamatwa jana  katika eneo la mkutano wa kura za maoni kwa tuhuma za kuhusika na rushwa katika mchakato wa kupatikana kwa mgombea wa chama chao.

Habari zinasema kukamatwa kwa meneja huyo kunatokana na madai ya kutotoa ushirikiano kwa maofisa wa Takukuru  waliokuwa wakimsaka mfanyakazi wa kituo hicho aliyetajwa kuwa ni Pili Sirikwa kwa tuhuma za kuhusika na ugawaji wa fedha katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa habari hizo maofisa wa Takukuru walikwenda katika kituo cha Radio Five kilichopo njiro kumtaka Sirikwa lakini uongozi wa kituo hicho ukamficha ndipo wakaamua kumtia mbaroni meneja huyo.

Juzi TAKUKURU walimkamata mfanyabiashara maarufu ya madini ya Tanzanite mkoani Arusha, diwani wa Kata ya Mbuguni, Arumeru, Thomas Mollel aka Askofu kwa tuhuma za kutoa rushwa na kushawishi madiwani kumpigia kura mmoja wa waliokuwa wagombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki.

Katika uchaguzi huo uliokuwa wa marudio uliwapambanisha Siyoi Sumari na Sarakikya ambapo hadi hatimaye Siyoi alitangazwa kuwa mshindi wa kura hizo baada ya kumshinda Sarakikya kwa kura zaidi ya silimia 50 zilizotakiwa.

Takukuru iliwakamata pia wanachama watatu wa CCM akiwemo Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Monduli Ezekiel Mollel kwa tuhuma hizo hizo.

Takukuru mpaka jana imeshawatia mbaroni watu sita wanne wakiwa tayari wametajwa majina yao na wengine majina yao kuhifadhiwa na  taasisi hadi itakapokuwa tayari kuyatoa.

Kamanda wa Takukuru Kasomambuto alisema 'Askofu' alikamatwa akiwa katika kikao cha baraza la madiwani akidaiwa kuhusika kuwashawishi wajumbe kwa rushwa.

Kasomambuto alisema askofu alikabidhiwa kushawishi kundi la madiwani wa jimbo la Arumeru Mashariki ili wampigie kura Siyoi Sumari ambapo juzi alikutana na baadhi katika kikao ambacho hakikua rasmi wala halali kwa wakati huu.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na Elirehema Kaaya ambaye awali alikuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo lakini alishindwa kwa kupata kura 205 kwani ilidaiwa kuwa naye alihusika kushawishi waliompigia awali kumpa kura Sioi katika uchaguzi wa marudio na mwingine aliyekamatwa ni Ezekiel Mollel ambaye ni katibu wa Jumuiya ya vijana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Monduli.

Takukuru imesema wote watatu inawashikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uchunguzi huo ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI