Mh. Edward Lowassa atembelea shule ya Mtakatifu Ann's mkoani Morogoro

Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.


Mh Lowassa aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi na viongozi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mtakatifu Anns iliyoko Morogoro.


Aidha Mh Lowassa alitoa zawadi ya mpira kwa kila darasa katika shule hiyo, ikiwa ni katika kuhamasisha michezo mashuleni.

Naye Mkuu wa shule hiyo Sister Dennis pamoja na wanafunzi na watawa wengine shuleni hapo walimtakia Mh Lowassa afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania.
Katika picha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha (kushoto) wakati akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa,Mama Regina Lowassa na wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo,Sista Dennis.
Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro. Chanzo Full Shangwe BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*