Muhimbili watoa mwili wa Muhindi kwa Waswahili

WAFANYAKAZI wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar wametoa mpya baada ya kuwapa ndugu mwili wa marehemu ambaye sio ndugu yao.

Ndugu wa marehemu walibaini kuwa mwili waliouchukua si wa ndugu yao bali ni wa mtu mwenye asili ya kihindi, muda mfupi kabla ya kufanya maziko jana, baada ya kuufikisha kijijini kwao mkoani Tanga.

Juzi usiku, ndugu hao walikwenda katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yao aliyefahamika kwa jina la Luku Mwaopea ambaye ni mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni wilayani hapa.

Kwa mujibu wa ndugu hao, walikabidhiwa bila kuutizama majira ya saa mbili usiku na hatimaye kuupakia ndani ya gari aina ya Toyota ukiwa umehifadhiwa katika jeneza na kuanza safari kuelekea kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza kwa maziko.

Ndugu hao baada ya kukabidhiwa mwili wa marehemu, walianza safari kuelekea wilayani Muheza ambapo walifika katika kijiji cha Mkanyageni jana asubuhi majira ya saa tatu.

Wakati wa hatua za mwisho za maandalizi ya maziko, ndipo ndugu wa marehemu walipobaini kwamba mwili waliopewa si wa ndigu yao, walipoanza kuutizama kwa heshima ya mwisho.

Kwa msgangao, ndugu hao walibaini kuwa wamepewa mwili wa Muhindi badala ya ndugu yao, suala lililozua mshangao kwa kila aliyekuwepo msibani hapo.

Baada ya tukio hilo ndugu wa marehemu wafanya mawasiliano na wahudumu wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili kuulizia mwili wao kama upo ambapo walijibiwa upo.

Hata hivyo safari ya kuurudisha mwili wa marehemu huyo mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika jina moja la Lukumai ilianza tena kwa ndugu kulazimika kuurejesha Dar es Salaam ili wakamchukue ndugu yao kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika tena leo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu huyo, Mwendo Abdallah alisema kuwa tukio hilo ni la kweli na kwamba lilitokana na makosa yaliyofanya wakati wa kukabidhiwa mwili huo huko Muhimbili.

Hata hivyo wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili walipoulizwa walisema kuwa marehemu hao wamefanana majina yao ambapo yule Muhindi anaitwa Lukumai na yule ndugu yao anaitwa Luku Mwaopea ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni kata ya Ngomeni wilayani Muheza.

Hata hivyo kwa sasa kaburi lililochimbwa lipo wazi kwa ajili ya mazishi ya kesho na kwamba viongozi wa chama na Serikali walihudhuria mazishi hayo na kushangazwa na hatua hiyo. Chanzo Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI