Mwanafunzi kidato cha Tano apotea Dar es Salaam

MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18), amepotea jijini humo.
Shangazi wa kijana huyo, Adelaide Kisongo amesema, Franco ni mgeni jijini Dar es Salaam amepotea tangu Jumapili asubuhi ikiwa ni siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kwa mujibu wa Adelaide, kijana huyo aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake Kariakoo, hakufika huko, na pia hakurudi shule na hadi sasa haijulikani alipo.
Amesema, walimu na walezi wa kijana huyo Mrangi, wametoa taarifa katika vituo vya Polisi Mbagala Kizuiani, Chang’ombe na Msimbazi, na wanatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.
Kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu mahali alipo kijana huyo anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha polisi au kuwasiliana na wenye namba zifuatazo za simu. 0784- 384035, 0717-371763, 0713- 761006, na 0715- 247544

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.