NHIF-Tumieni fedha za CHF kununulia dawa

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Erasto Mbwiro akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Manyara jana.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
Mwanaidi Mtanda akitoa salaam za
Bodi kwa wadau wa Mfuko katika
Mkutano uliofanyika Mkoani
Manyara leo.
.Naibu Mkurugenzi Mkuu waMfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis
Mdee akifafanua jambo wakati wa
kutoa msaada wa mashuka 150
katika Hopsitali ya Halmashauri ya
Mji wa Babati kama mchango wake
ndani ya jamii, kulia ni Mjumbe wa
Bodi ya NHIF, Mwanaidi Mtanda.
Kikundi cha waendesha piki piki
mkoani Arusha wakiwa wamevalia
makoti ya usalama barabarani
yaliyokabidhiwa na NHIF baada ya
kujiunga na CHF.

Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na
Uwekezaji, Deusdedit Rutazaa akitoa
mada kwa wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya mkoani Manyara
jana.
.Wagonjwa wakiwa wamefunikwa
mashuka yaliyotolewa na NHIF
katika Hospitali ya Maunt Meru,
Arusha muda mfupi baada ya
kutolewa kwa msaada huo.
Wadau wa NHIF mkoani Manyara
wakifuatilia mada katika mkutano
wa siku ya wadau.

NHIF; Tutaongeza wigo wa wanachama
Na Mwandishi Wetu, Manyara
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema kuwa utahakikisha unaongeza wigo wa wanachama kwa kuimarisha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kutimiza lengo lake la kufikia asilimia 30 ya Watanzania kuwa kwenye utaratibu wa Bima ya Afya ifikapo 2015.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Fedha Mipango na Uwekezaji Bw. Deudedit Rutazaa wakati akiwasilisha mada ya utekelezaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya tangu uanzishwe mwaka 2001 kwa wadau wa Mfuko huo mkoani Manyara.
Alisema kuwa ili kufikia lengo hilo, Mfuko utavihusisha Vikundi mbalimbali, vyama vya Ushirika, shule na vingine lakini pia kuishauri Serikali kubadili sheria iliyopo.
"Tutaendelea kuwekeza katika miradi ya uboreshaji wa huduma za afya kwa kuwa na vituo vya mifano katika mikoa mingine hususan iliyoko pembezoni, tutaimarisha utendaji wa Mfuko kwa kusogeza zaidi huduma kwa wanachama wetu hasa kufungua ofisi kwenye mwaka wa fedha 2012/2013 na kupanua zaidi wigo wa huduma kwa wanachama wetu kwa kuwawezesha kupata huduma ndani ya Afrika Mashariki," alisema Rutazaa.
Alisema kuwa ili hayo yaweze kufanikiwa ni vyema sasa wadau wote wakaelewa haki na wajibu wao katika Mfuko ili waweze kuelimisha wananchi wengine kujiunga na Mifuko ya NHIF na CHF.
"Jambo jingine tungewaomba sana viongozi kusimamia matumizi ya fedha ambapo sisi kama Mfuko tutatoa taarifa za utekelezaji kwenye uongozi wa Mkoa na Wilaya kila robo ya mwaka na kuziwasilisha katika Baraza la Madiwani, fedha hizi zikitumika vizuri zitachangia kwa kiwango kikubwa kuboresha huduma kwa wanachama wetu na kwa wananchi kwa ujumla," alisema Rutazaa.
Hata hivyo wakati akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Erasto Mbwiro alizitaka Halmashauri kuangalia uwezekano wa kuwa na sheria zitakazowalazimisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.
Alisema kuwa Mfuko huo wa Afya ya Jamii hauwezi kuwa na mafanikio ya kutosha endapo hapatakuwa na sheria inayomlazimisha mwananchi kujiunga nao hivyo akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuliangalia hilo kwa makini ili liweze kufanikiwa.
"Hakuna mtu anayependa kuumwa na ugonjwa unakuja wakati ambao hata hela hauna hivyo ni lazima huu Mfuko tuuchangamkie ili wananchi wetu wapate uhakika wa matibabu ...bila afya njema hakuna maendeleo na maadui umasikini na ujinga ndiyo yatapata nafasi," alisema Mbwiro.
Pia alizitaka Kamati za Afya na Elimu kuhakikisha zinafanya kazi ya kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Mfuko huu ili wajue faida zake na wahamasike kujiunga nao.
"Haiwezekani Manyara tukawa kwenye asilimia tatu ya kaya zote zilizoko mkoani hapa na wakati kila kaya ina mifugo ya Ng'ombe na kuku...na mchango wa Mfuko huu ni kati ya elfu kumi au shirini ambazo zinaweza kutokana na kuuza hata kuku mmoja tu hivyo ni lazima tujipange,' alisema Mkuu huyo.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA