NHIF YATOA MSAADA WA MASHUKA SH.MIL 7 VITUO VYA AFYA KILIMANJARO

 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (wa kwanza kushoto), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimnanjaro Bi. Ruth Malisa ( mwenye kilemba) wakiwa wameambatana na maofisa wengine wa Mfuko huo wakipata maelezo  kutoka kwa Mtaalam kutoka Wakala wa Majengo (TBA) juu ya jengo la upasuaji ambalo linajengwa katika Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi na ambalo kwa sasa limesimama baada ya kukosa pesa na jitihada zinaendelea kupata fedha za kuliendeleza. Bw. Mdee alipata nafasi ya kuelezea Uongozi wa Mkoa na Hospitali kuhusu Mikopo ambayo NHIF inatoa kwa ukarabati wa majengo na ununuzi wa vifaa tiba kwa vituo vilivyosajiliwa na Mfuko ambayo wanaweza kuitumia kama chanzo kimojawapo katika kupata fedha za kuendeleza mradi huo. Kwa mujibu wa Mtaalam huyo, ili likamilike jengo hilo linahitaji Shilingi Bilioni 1.5 na litakuwa na uwezo wa kuendesha upasuaji kwa watu watatu kwa wakati mmoja.



 
Katika maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mfuko umekuwa ukiendelea kufanya mikutano ya wadau katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Pamoja na hayo Mfuko umekuwa ukitembelea viongozi wa Mikoa na Vituo vya Afya ili upata ripoti mbalimbali na kujadili uboreshaji wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko. Pichani Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Mfuko wakijadili mambo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimnanjaro Bi. Ruth Malisa na viongozi wengine wa Mkoa jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Mfuko huo unategemea kuwa na Mkutano wa wadau mjini Moshi siku ya Jumatatu 2/4/2012.

 Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi imetenga jengo maalum kwa ajili ya kuwahudumia Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Pichani Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Kapalala Saganda ambapo alisema hii ni katika hatua za kuboresha huduma kwa wanachama hao. Sehemu hiyo ina nafasi ya vyumba vitatu vya madaktari, maabara, chumba cha dawa na vyumba vya matibabu. Alisema jambo hili limesaidia sana kuboresha huduma kwa wanachama na wamedhamiria kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama hao.
 
Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akikabidhi mashuka 150 kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Ruth Malisa wakati alipotembelea Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro jana 31/3/2012. Hospitali hiyo imesajiliwa na Mfuko huo na inahudumia wanachama wa Mfuko. Mshuka hayo ni sehemu ya mashuka 700  yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 ambayo Mfuko huo unayatoa kwa Vituo vya Afya vya Mkoa huo kama sehemu ya kuihudumia jamii katika maadhimisho ya Miaka Kumi ya Mfuko huo.

 

Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akikabidhi mashuka 150 kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Ruth Malisa wakati alipotembelea Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro jana 31/3/2012. Hospitali hiyo imesajiliwa na Mfuko huo na inahudumia wanachama wa Mfuko. Mashuka hayo ni sehemu ya mashuka 700  yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 ambayo Mfuko huo unayatoa kwa Vituo vya Afya vya Mkoa huo kama sehemu ya kuihudumia jamii katika maadhimisho ya Miaka Kumi ya Mfuko huo.

 





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.