NI KIPINDI CHA PILI SIMBA INAONGOZA 2-0 DHIDI YA AFRICA LYON, HUKO MKWAKWANI TANGA YANGA-0 NA COASTAL-0 MPIRA KIPINDI CHA PILI

 Mchezaji wa timu ya Africa Lyon Khamis Yusuf akiukokota mpira huku mshambuliaji wa timu ya Simba Felix Sunza akimfukuzia kwa nyuma ili kunyang'anya mpira huo katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika kwenye uwanja na Taifa jijini Dar es salaam jioni hii.
Hivi sasa ni kipindi cha pili na timu ya Simba inaongoza magoli 2-0 dhidi ya timu ya Africa Lyon yaliyofungwa na mchezaji Salum Machaku alliyepiga mpira wa kona uliombabatiza golikipia wa timu hiyo na kuingia moja kwa moja nyavuni, goli la pili la Simba limefungwa na Mshabuliaji Haruna Moshi Boban.
Wakati huohuo huko Tanga timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam inamenyana na timu ya Coastal Union ya huko na sasa hivi ni kipindi cha pili, hata hivyo hakuna timu iliyokwishapata goli
Mashabiki wa timu ya Simba wakishagilia kwa nguvu wakati timu hizo zikicheza uwanjani. Chanzo Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.