OBAMA AZURU MPAKA WA KOREA KUSINI NA KOREA KASKAZIN

Rais Barack Obama akiwa ziarani Korea Kusini, amezuru eneo la mvutano la mpaka na Korea Kaskazini.
Amewasili Korea Kusini kwa mkutano wa kilele kuhusu usalama wa silaha za nuklia, ikiwa sehemu ya mpango wake wa miaka mine kuzuwia zana za nuklia kufika katika mikono ya wahalifu.
Rais Obama alizuru kituo cha ulinzi karibu na eneo linalotambuliwa na jeshi kuwa linatenga Korea Kaskazini na Kusini.
Alitumia darubini kuangalia vijiji ndani ya taifa la kikoministi la Korea Kaskazini.
Hapo awali, alisimama mbele ya wanajeshi wa Marekani, na kuwaambia kuwa wako zamu kwenye "mpaka wa uhuru".
Shughuli hizo alizofanya leo asubuhi, baada ya kuwasili tu Korea Kusini, zimekusudiwa kuwaunga mkono wanajeshi wa Marekani walioko huko na kuonesha ushirikiano wa kijeshi baina ya Marekani na Korea Kusini.
Piya zinaonesha mvutano ulioko hivi sasa na Korea Kaskazini yenye silaha za nuklia.
Korea Kaskazini haitahudhuria mkutano huo wa kilele mjini Seoul.
Mazungumzo nje ya mkutano yanaelekea kuhusika hasa na hitilafu mpya kati ya Marekani na Korea Kaskazini, kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kurusha satalaiti angani mwezi ujao.
Wakuu wa Marekani wamesema wazi kuwa Rais Obama atalizusha swala hilo kwenye mazungumzo yake na marais wa Uchina na Urusi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI