Ofisi ya Bunge yapokea rasmi nyumba mpya ya Spika

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas Wambura mara tu kabla ya makabidhiano rasmi ya jengo la nymba atakayokuwa anatumia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoko eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.
Muonekano wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo litakuwa makazi ya Spika yeyote atakayeliongoza Bunge la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 na limegharimu takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika wa Bunge Dodoma
Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction Company ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban Mwatawala (kulia) akitoa maelezo ya ujumla kabla ya kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya Bunge katika jengo hili. Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha Bw. Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na Teknolojia ya Mawasiliano wa Bunge Bw. Siegfied Kuwite, na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John Joel.
Bw. Siegfried Kuwite akitia saini makabidhiano hayo kwa niaba ya Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mshitiri (client) wa jengo.
Bwana Mwatawala akimkabidhi Msanifu Majengo M. F. M Msangi (kulia) anyewakilisha Wakala wa Majengo ya Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa Mradi huu.
Timu nzima iliyoshiriki katika makabidhiano hayo.
Picha zote na Prosper Minja-Bunge

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA