PINGAMZI LA TUNDU LISU DHIDI YA KESI YA KUPINGA UBUNGE WAKE YAGONGA MWAMBA

IFUATAYO NI TAARIFA FUPI YA KAWAIDA JUU YA PINGAMIZI LILILOWEKWA NA MHE. TUNDU LISSU MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI KWENYE KESI NO 1 YA MWAKA 2010 INAYOPINGA USHINDI WAKE 

UTANGULIZI:
Kesi hii ilifulinguliwa na: 
1.       Shabani Itambu Selema,
 2.       Pascal Marcel Hallu.
Dhidi ya
1.       Tundu Antiphas Mghwai Lissu

2.       The Returning Officer Singida mashariki constituency
3.       The Attorney General

KIINI CHA KESI.
Katika kesi hii walalamikaji wanapinga ushindi alioupata Mhe. Tundu lissu kwa madai kuwa ushindi huo haukutokana na uchaguzi huru na haki kwani sheria zinazosimamia uchaguzi zilikiukwa.

HOJA ZA PINGAMIZI:
Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hii Mhe. Tundu Lissu aliweka hoja saba za kisheria za pingamizi.
Kiujumla alidai kuwa madai yaliyofunguliwa yalikuwa na mapungufu ya kisheria kama ifuatayo:
1.       Ada yakulipia (Petition) madai hayo ilikuwa 12500 badala ya 200,000/= inayotakiwa kwa mujibu washeria (Election rules za 2010)
2.       Kwamba baadhi ya vipengele vya madai hayo vilikuwa jumla mno havikufafanuliwa wazi, vilikuwa vinachefua na kwamba ni ngumu kujibu vipengele hivyo.
3.       Alidai kuwa kiapo (Affidavit)ya mlalamikaji wa pili ilikosewa.
4.       Alidai kuwa mambo ambayo walalamikaji waliiomba mahakama iwafanyie kama wanashinda kesi (Reliefs) hayakuzingatia matakwa ya sura ya 112 ya sheria ya uchaguzi.
5.       Alidai  kuwa baadhi ya maofisa waliotuhumiwa hawakuuganishwa katika mashtaka kama sheria inavyoelekezwa.
NB:Kwa ujumla mambo makubwa ni hayo.

MAJIBU YA HOJA HIZO.
Wakili wa walalamikaji Ndugu Wasonga alitoa ufafanuzi wa kina juu ya hoja zote.
1.       Kuhusu kulipa ada pungufu alieleza kuwa msajiri ndiye anayefanya makisio ya  kiasi cha ada ambacho hulipwa. Alicholipa kilikisiwa na mahakama.
Lakini pia alirejea maamuzi ya mahakama ya Rufaa ya Tanzania.
Alisema kuwa,Kulipa ada pungufu hakuondolei mahakama uwezo  wa kusikiliza kesi, mahakama inaweza kuwaagiza  upande uliolipa ada pungufu kulipa ada kamili.
2.       Kwa hiyo ombi hilo au pingamizi hilo limeshindwa.
3.       Kuhusu vifungu vinavyodaiwa kutofafanuliwa vizuri.
Pamoja na utetezi uliotolewa  na mahakama imeamuru baadhi ya vifungu vifutwe ambavyo ni kifungu cha 7,8,11,12,13 na 18.
Pamoja na kufutwa vifungu hivyo bahati nzuri madai yote ya msingi yamebaki pale pale kwa hiyo kufutwa kwa vifungu hivyo hakujaathiri madai ya msingi.

MAAMUZI YA MAHAKAMA
·         Mahakama imeamuru ada iliyobaki ilipwe ambayo ni 187,500/= ndani  ya siku moja yaani tarehe 15/3/2012.
·         Hati ya madai ifanyiwe marekebisho (amendment) viondolewe vifungu hivyo tu. Kusifanyike marekebisho mengine kabla ya tarehe 15/3/2012.
·         Majibu yawadaiwa nayo yarekebishwe ili vifungu viendane kusifanyike marekebisho mengine 16/3/2012.
·         Preliminary Hearing (P.H) itaendelea tarehe 19/3/2012.

UMBEYA.
·         Wapenzi wa Chadema walijiandaa kusherekea lakini waliondoka kama kuku aliyelowa.
·         Kesi bado ni ngumu kwa Tundu Lissu.
·         Baada ya maamuzi hayo ukimya ulitawala

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA