POLISI IRINGA WASEMA RUKSA WANAHABARI IRINGA KUANDAMANA KESHO

Mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambaye pia ni naibu katibu mkuu chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) kushoto akiwa ameongozana na mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi ,Mtangazaji wa Nuru FM Bw.Sagi na mtangazaji wa Ebony Fm George Ndamagoyo kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa leo baada ya kuomba kukutana bila kuafikiana .
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limebariki maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa yaliyopangwa kufanyika kesho majira ya saa 4 asubuhi katika mji wa Iringa. Katika kibali hicho kilichotolewa na jeshi la polisi leo asubuhi kabla ya kutolewa lilikutana na katibu wa IPC Frank Leonard kuomba kufanya marekebisho ya njia na kukubaliana na kuifuta njia ya Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda barabara ya samora na kuishia kanisa la RC mshindo na baada ya hapo kurudi kwa kupita barabara ya Mashine tatu ,Stendi kuu ,M.R Hoteli na kuishia ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. Katika barua hiyo ya jeshi la polisi yenye kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa kwa mtendaji mkuu wa Iringa Press Club yenye kichwa cha Maombi ya kibali cha kufanya maandamano ya amani . Imeanza kwa kusema tafadhali rejea barua yako kumb. IPC/02/o12/ Machi 2 ya 03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu. Kibali kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya wanahabari mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4 asubuhi kama ifuatavyo maandamano hayo yataanzia kwenye bustani ya manispaa ya Iringa kuelekea kanisa la Mshindo kwa kupitia barabara ya Uhuru. Baada ya kufika kanisa la Mshindo watapita barabara ya Ubena Club kuelekea stendi kuu ,MR Hotel,Luxury hadi ofisi za mkuu wa mkoa ambapo yataishia . Nakala kwa RPC Iringa kwa taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo Nawatakia maandamano mema Mkuu wa polisi wilaya ya Iringa MOhamed Mkwazu Semunyu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU