RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Rais wa chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Nchini Dk. Rachel Mhavile baada ya kumkabidhi tuzo kutokana na juhudi zake za kuhamasisha masuala ya kinywa na meno ndani na nje ya nchi . Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma ambapo jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wanahudhuria mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo. Jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wanahudhuria mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo. Jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Nchini Dk. Rachel Mhavile (kulia) na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donnan Mmbando baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma ambapo jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete amesema kwamba serikali itafanya kila iwezavyo katika kupanua na kuendesha huduma za afya zilizobora na kisasa ili kuhakikisha taifa linakuwa la watu wenye afya njema kwa kuzuia na kutibu magonjwa mbalimbali katika kipindi cha uongozi wake.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais Kikwete mara baada ya kukabidhiwa kadi ,katiba na tuzo ya kukubali kuwa mwanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na Rais wa chama hicho, Rachel Mhaville katika hoteli ya Court yard jijini DaresSalaam.
“Sikutegemea kutokea kwa kitendo hiki. Ninachoweza kusema ninaomba mniamini nitakuwa mwanachama mzuri. Tutafanyakazi kwa pamoja ili kutimiza ndoto zenu hususan kuhakikisha mradi wa kituo cha Kigamboni cha magonjwa hayo unaanzishwa.
“Hili ni jukumu kwangu , kwani lengo langu ni kuliacha taifa likiwa lenye watu wenye afya njema,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa serikali yake inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha ujenzi wa Chuo Kikuu kipya cha Sayansi za Afya na Tiba eneo la Mlongazila unafanikiwa ili kiweze kufanya kazi kabla ya mwaka 2015.
Rais Kikwete alisema chuo hicho kitakuwa na shule mbalimbali za afya na tiba.
Akifungua mkutano wa mafunzo ya siku tatu ya kuweka hatua za awali za kupata huduma za kuzuia na kutibu magonjwa hayo, Rais Kikwete alisema bado kuna safari ndefu ya kuiwezesha sekta ya huduma hiyo kuwa na rasimali watu wa kutosha wakiwemo madaktari, wauuguzi na watumishi wengine wa eneo hilo.
Rais Kikwete aliongeza kuwa sekta hiyo ina upungufu wa madakatari ukilinganisha na idadi ya watu nchini wapatao milioni 43 .
Alizitaja takwimu za madaktari wa sekta hiyo nchini kuwa wapo 518 ambapo uwiano unaonesha kuwa 1: 120,000 (yaani daktari mmoja kwa wagonjwa 120,000) wakati kwa sheria za Shirika la Afya la Dunia(WHO) 1:7500 (yaani daktari mmoja anatakiwa kutibu wagonjwa 7500).
“Serikali itaendelea kujenga uwezo kwenye hospitali na kituo cha afya, lazima ziwe na vitengo vya huduma za kinywa na meno,” alisisitiza huku akiongeza kwamba itasaidia kuanzisha na kupanunua vilivyopo na itangalia ili iweze kuanzisha hata katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Alitoa changamoto kwa wadau wa sekta hiyo kuhakikisha kuwa huduma za magonjwa hayo zinapatiakana, kutolewa katika hatua za awali na kwa gharama nafuu.
Naye Rais wa chama hicho, Mhaville alisema aliitaka jamii kuacha kutembea na magonjwa hayo badala yake wafike hospitali ili kupata ushauri na tiba kwa kuwa magonjwa hayo yanazuilika.
Alisema changamoto iliyopo kwao ni kutoa elimu kwa jamii hususan kwenye maeneo ya vijijini.
Mhaville alisema mkutano huo utatengeneza mwongozo wa mamna ya kuyashughulikia magonjwa ya afya ya kinywa na meno, ambapo Rais alisema serikali inausubiri kwa hamu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.