RAIS KIKWETE AWASILI MJINI MOSHI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi jioni hii.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILINO YA RAIS
MARCH 4, 2012
MOSHI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI