Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein
---
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

MKUU WA KIKOSI CHA VALANTIA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 9(1) cha sheria ya Kikosi cha Valentia,Zanzibar No.5 ya mwaka 2004,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua LT. COL. Mohammed Mwinjuma Kombo kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valentia,Zanzibar.

KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 76(1) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi,Zanzibar.

MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) (a) cha Sheria ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Zanzibar No.8 ya mwaka 2011, Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Abdulghan Himid Msoma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamalaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar.

MWENYEKITI WA BARAZA LA ELIMU, ZANZIBAR.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1) cha Sheria ya elimu No.6 ya mwaka 1982 kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 6 cha sheria No. 4 ya Mwaka 1993 Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Saada Thani Fakih kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu,Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza 25 Machi 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA