SBL YACHANGIA MIL 10 TUZO ZA EJAT


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) akifafanua jambo katika mkutano huo kuhusiana na udhamini wao katika tuzo hizo, kulia ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, ambalo limesaidia sana MCT kupata udhamini huo.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tuzo za waandishi wa habari (EJAT) itakayofanyika hivi karibuni, pamoja na waandishi wa habari wakati akishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kufuatia msaada wa shilingi milioni 10.925.000 ilioutoa kwa baraza hilo kwa ajili ya maandalizi ya tuzo hizo, katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya baraza hilo Mwenge jijini Dar es salaam, katika picha katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 10.925.000 kwa Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT) , fedha ambazo Kampuni ya (SBL) imetoa kwa Baraza la Habari (MCT) kwa ajili ya kufanikisha tuzo hizo, katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.