SBL YAZINDUA MRADI WA KUVUNA MAJI YA MVUA HOSPITALI YA WILAYA IRINGA

Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) akizungumza na waansdishi wa habari hawapo pichani baada ya uwekajiwa jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa.
Naibu Waziri wa Maji Injinia Gryason Rwenge akiweka jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna majiya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Dk. Stella Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa hospitali hiyo na Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa (SBL).
Hii ndiyo Hospitali yenyewe na hawa ni baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo mara baada ya kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi.
Wafanyakazi wa mradi huo wakichimba msingi wa kuweka matanki hayo.
Mradi huo kuwezesha zaidi ya watu 150,000 kupata maji safi na salama
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation leo imezindua mradi wa uvunaji maji katika hospitali ya Frelimo ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012.
Zaidi ya watu wapatao 150,0000 wanaohudumiwa na hospitali hiyo watanufaika. Maadhimisho ya wiki ya maji nchini Tanzania yafanyika kitaifa mjini Iringa.
Mradi huu wa uvunaji wa maji ya mvua ulifikiwa baada ya kushauriana na Wizara ya maji na Manispaa na kutambua wingi wa maji yanayopotea ambayo yangeweza kuvunwa kwa matumizi.
Mradi unatarajiwa kutumia kiasi cha zaidi yashilingi milioni 50 ikiwa ni gharama za ununuaji na uwekaji wa matanki ya maji, mabomba, pampu ya umeme na ukarabati mdogo wa miundo mbinu iliyopo.
Kampuni ya bia ya Serengeti inafahamu na inatambua umuhimu wa maji duniani na hata katika biashara yetu, na ndio maana basi tunashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama.
Kwa mwaka huu pekee Kampuni ya Bia ya Serengeti imetenga zaidi ya shilingi milioni 300 katika miradi ya maji.Kati ya hizo, shilingi milioni 100 ni kwa ajili ya udhamini wa wiki ya maji ambazo zimetumika katika matangazo , mabango ya matangazo , fulana, kofia , vipeperushi , vijarida n.k.
Kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni kwa ajili ya miradi endelevu ya maji katika mikoa ya Iringa , Mwanza, Moshi na Dar es Salaam.
Kama kampuni inayowajika ,tumekuwa tukijihusisha na miradi mbalimbali ya maji safi na salama ukiwemo ule Mkuranga. Na pia tumeshiriki katika mradi wa kuboresha maji katika Hospitali Amana kwa kushirikiana na makampuni mengine na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Katika mradi wa Mkuranga , Kampuni ya Bia ya Serengeti imewekeza zaidi ya shilingi milioni 384.6 ambapo zaidi ya watu 250,000 wananufaika na mradi huu.
Kampuni ya Bia ya Serengeti itaendelea kufadhili miradi endelevu ya kuisadia jamii hasa miradi ya maji, ili kwa pamoja tuweze kupunguza na kuboresha miundombinu na upatikanaji wa maji safi na salama. Chanzo Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.