SIOI ACHUKUA FOMU TUME YA UCHAGUZI

Mgombea mteule wa CCM  jimbo la Arumeru Mashariki leo amechukua fomu Tume ya Uchaguzi kuomba kuteuliwa kuwa mgombea.

Taarifa zilizopatikana zimesema mgombea huyo Sioi Sumari (Pichani) amechukua fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi bila shamra shamra.

Haikuelezwea sababu zilizomfanya Sioi chukua fomu kwa staili hiyo, lakini wadadisi wa mambo wamesema huenda amefanya hivyo kwa sababu si kipindi kirefu tangu Baba yake mzazi wa mgombea huyo, Jeremia Sumari kufariki dunia.

Uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki unafanyika kufuatia kicho cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo hadi jana wagombea wa vyama vingine kikiwemo CHADEMA wamekwishachukua fomu kwa Msimamizi huyo wa uchaguzi.

Mgoimbea wa Chadema Nassari Joshua yeye alichukua fomu yake jana.

Kampeni za uchaguzi huo utakaofanyika Aprili mosi mwaka huu, zimepangwa kuanza kwa vyama vyote machi 9, mwaka huu, kiasi cha siku tatu zilizobaki kuanzia leo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU