Wanahabari Iringa wapanga kufanya maandamano ya amani

Na Francis Godwin,Iringa WANAHABARI mkoani Iringa wamepanga kufanya maandamano ya amani siku ya jumanne kupinga hatua ya uongozi wa mkoa wa Iringa kutumia ziara za viongozi wa kitaifa kunyanyasa wanahabari . Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya uongozi wa mkoa kuwalaza nje wanahabari hao wakati wa ziara ya Rais Kikwete wilaya ya Njombe na ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghirib Bilala aliyefanya ziara yake katika wilaya ya Makete ,Njombe ,Mufindi na Iringa hivi karibuni. Akitoa taarifa mbele ya wanahabari katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa leo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi alisema kuwa wanahabari wamekuwa ni watu wa kutetea makundi mbali mbali katika jamii ila wao wamekuwa nyuma kujitetea hata pale wanaponyanyasika . Hivyo alisema wakati umefika kwa wanahabari kuanza kufunguka na kudai haki zao pale zinapoonekana kupokwa na watu wachache kwa masilahi yao . Kwani alisema mkoa wa Iringa na vyombo vyake umekuwa ukiongoza kwa kuvibagua vyombo vya habari wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na wakati mwingine kuwataka wanahabari hao kuchangia gharama za ziara hizo iwapo wanataka kushiriki ziara husika . Mwangosi alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia afisa habari wake Denis Gondwe kutoa mialiko kwa wanahabari hasa pale mkoa unapohitaji kufikisha taarifa mbali mbali kwa wananchi ila inapotokea ziara za viongozi wa kitaifa ama mkuu wa mkoa kufanya ziara amekuwa akibagua vyombo vya habari na kutumia chombo cha serikali pekee Alisema katika ziara ya Rais Kikwete waandishi waliopata kushiriki ziara hiyo walinusurika kulala kwenye gari kabla ya paroko kuwatafutia vyumba ila katika ziara ya juzi ya makamu wa Rais pia mkoa ulitoa usafiri huku ukitaka waandishi hao kuomba fedha za kugharamia ziara yao kutoka katika vyombo vyao hali iliyopelekea wanahabari hao kukosa maeneo ya kulala wala kula wakati wote wa ziara hiyo. "Mkuu wa mkoa anapaswa kufanya kazi katika wilaya zote za mkoa wa Iringa kwa mshahara anaulipwa kila mwezi ......ila leo mkuu wa mkoa ama kiongozi yeyeto wa wilaya ama mkua anapofanya ziara katika eneo lake anajilipa posho ila mwanahabari anapoongozana na viongozi hao anaambiwa alipiwe na chombo chake kwa kazi ya ofisi ya mkoa"huu ni unyanyasaji mkubwa Kwani ni kweli vyombo vy habari vinatoa fedha kwa wanahabari wao kwa ajili ya kwenda kuandika habari zile ambazo chombo cha habari inazihitaji kwa wakati huo mfano kama kuna ufisadi umefanyika katika Halmashauri husika ama kuna ajali /maafa yametokea ila sio kwa kwenda kushiriki ziara ya mkuu wa mkoa. Alisema kuwa umefika wakati wa wanahabari mkoa wa Iringa kugoma kutumiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa badala ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waajiri wakuu wa wanahabari hao. Kuhusu maandamano hayo alisema kuwa yamepagwa kuanzia viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa na kupita mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kwa kuelekea uwanja wa Samora kabla ya kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa . Hata hivyo Mwangosi alisema wanahabari hao wataandamana wakiwa wamefunga midomo yao kwa plasta huku gari ya muziki likifuata kwa nyuma likiwa na wimbo maalum wa kudai uhuru maarufu kama ' Freedom is Coming Tomorrow' Alisema kuwa wanahabari mkoa wa Iringa wamechoshwa kunyanyaswa na ofisi ya mkuu wa mkoa na mara nyingi ofisi hiyo ya mkuu wa mkoa wa Iringa imekuwa ikidai kuwa serikali haina pesa jambo ambalo kimsingi ni sawa na kuishusha heshima serikali ya Tanzania . Mwangosi alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa imekuwa ikidai haina fedha za kulipia malazi na chakula kwa wanahabari huku msafara mfano wa makamu wa Rais ukiwa na magari zaidi ya 35 na viongozi wote katika magari hayo hadi madereva walilipwa posho ila wanahabari na askari polisi waliambiwa serikali haina pesa za kuwalipa Aidha alisema kuwa katika maandamano hayo wanahabari watatoa tamko lao pamoja na mapendekezi kwa ofisi ya mkuu wa mkoa kama itaona kuna haja ya kudumisha mahusiano yake na wanahabari ama kupuuza .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.