Wanajeshi walia TFF kuwapa hundi feki

UONGOZI wa klabu ya Ruvu Shooting umesema unasikitishwa na kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwapa hundi 'feki' na kukaa kimya kuwalipa Sh 5 milioni wanazodai tangu mwaka 2010.

Akizungumza kwa simu kutoka Ruvu mkoani Pwani jana, meneja wa Ruvu Shooting, Narcis Ndunguru alisema kuwa fedha wanazodai ni zile zinazotolewa na wadhamini kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kwaajili ya kugharimia usafiri na malazi.

"Ndugu hapa tunapoongea tunaidai TFF sh5,447,500 za usafiri na malazi tangu mwaka 2010 wamekuwa wakitupiga danadaga tu.

"Tunashangaa kwanini hawatulipi wakati ni haki yetu, lakini kama wadhamini wanatoa hela zinaenda wapi?.,"alisema Ndunguru.

Alifafanua zaidi kwa kusema kuwa awali Novemba 3, 2011,TFF iliikabidhi klabu hiyo hundi yenye namba 981944, lakini chakusikitisha ni kwamba walipoipeleka benki waliambiwa ni feki na ndipo walichukua jukumu la kuirudisha ingawa alidai tangu wakati shirikisho hilo halijawalipwa zaidi ya kuwazungushwa.

"Hawajamaa wametuzungusha sana, kila siku njoo kesho njoo kesho, kifupi ni kwamba awaliTFF ilipotupa hundi hewa, hii ilibainika baada ya kuipeleka benki Novemba 18, 2010, kinachoshangaza inakuaje tupewe hundi feki? na kama akaunti yao ilikuwa haina hela kwanini waliitoa,ili ni kosa kubwa,"alisema Ndunguru.

Aliongeza kuwa Agosti 27 mwaka jana waliiandikia barua TFF kuwakumbusha juu ya deni lao ambapo waliahidiwa kulipwa ingawa alidai ahadi hiyo pia haijatekelezeka mpaka sasa.

"Baada ya ukimya wao tuliwandikia barua lakini waendeleleza sera ile ile ya tutawalipa sasa mpaka lini wakati na sisi tunamipango yetu?.,"alihoji Ndunguru

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alipotafutwa ili aweze kujibu malalamiko hayo ya Ruvu Shooting alisema wenye nafasi nzuri ya kulizungumzia ni kamati ya ligi ingawa jitihada za kumsaka mwenyekiti wa kamati hiyo Wallace Karia ili atoe ufafanuzi wa suala hilo ziligonga mwamba huku simu yake ya mkononi ikiita bila majibu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.