Wizi wa ngawira waendelea Mali

Kiongozi wa mapinduzi ya Mali, ametoa wito ghasia na wizi wa ngawira umalizike.
Siku ya tatu ya mapinduzi, Kepteni Amadou Sanogo alitokeza kwenye televisheni kuzima uvumi kwamba ameuwawa.
Kuna mtafaruku katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Wizi wa ngawira unaoendelea na uhuni umewafanya wakuu wa kijeshi kutoa wito mwengine kuwa watu wawe watulivu.
Kepteni Amadou Sanogo, kiongozi wa mapinduzi, ametokeza kwenye relevisheni ya taifa kuomba msamaha kwa wizi wa ngawira unaofanywa na wanajeshi wa daraja za chini, na wale aliowaita watu wasiokuwa na nia njema.
Alisema vitendo hivyo siyo kazi wala azma yao.
Kepteni Sanogo piya alikanusha tetesi kwamba aliuliwa jana usiku, na kwamba njama nyengine ya mapinduzi inapikwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Amadou Toumani Toure.
Inaelekea maafisa wa vikosi vengine vya jeshi walikuwa wamemzunguka Kepteni Sanogo wakati wa hotuba yake hiyo kwenye televisheni, kuonesha kuwa jeshi liko pamoja na linaunga mkono mapinduzi hayo.
Inafikiriwa kuwa Rais Toure bado analindwa na kikosi maalumu na hakuna hakika kuwa jeshi zima sasa linamuunga mkono kiongozi mpya.
Muungano wa vyama vikuu vya upinzani, umelaani mapinduzi hayo, na umetaka uchaguzi ufanywe.
Uchaguzi ukitarajiwa kufanywa mwisho wa mwezi huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*