14 WAJITOKEZA REDDS MISS KURASINI 2012




Miss Kurasini anaeshikilia taji ambaye pia ni Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

SHINDANO la Redds Miss Kurasini 2012, ambalo linataraji kufanyika Mei 25 mwaka huu katika ukumbi wa Equator Grill, yamezidi kupata wadhamini watakaofanikisha shindano hilo.

Akizungumza jana Mkurugenzi wa ZUM Fashion & entertainment, Zuwena Mustapha amesema mbali na Kampuni ya Bia Tanzania kudhamini shindano hilo kupitia kinywaji chake cha Redds, pia makampuni kadhaa yamevutiwa na kuamua kudhamini shindano hilo.

“Leo napenda kuwaambia kuwa hadi sasa tunajumla ya wadhamini 14 ambao wamejitokeza kudhamini shindano hilo, lakini bado milango ipo wazi kwa yeyote anaependa kutuzamini na kusaidia warembo wetu wa kurasini kupata zawadi nono na shindano kuwea zuri,”alisema Mustapha.

Mustapha amesema wadhamini wakuu wa shindano hilo ni Nameems Wear wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.

Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20),Linda Deus (20),Irene Sostheness 20),Neemadoree Sylvery(29),Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22)      na Sia Kimambo (19).

Shindano hilo la Urembo ya Miss Tanzania katika kituo cha Kurasini yanategemea kupambwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao watatangazwa hivi karibuni.  

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU