Hivi ndivyo Fusu hilo lilivyokuwa baada ya ajali
Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewa
Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
Wananchi wakitazama Fuso ambalo liligongana na Taxi hiyo
skari wa usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya asubuhi hii
Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo
Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo .Mashuhuda waliozungumza na Mdau Francis Godwin wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi am,bako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea .
Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .
Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .
Comments