Extra Bongo yamlilia Mwiligwa


Na Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki wa dansi Extra Bongo Next Level imeungana na familia na wanahabari wote nchini kuomboleza kifo cha Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa kilichotokea usiku wa kuamkia Ijumaa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa bendi hiyo, 'Kamarade' Ally Choki, Extra Bongo imepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Rachel kutokana na kutambua na kuthamini mchango wake alioukuwa akiutoa katika harakati zake za kupigania kurudisha ushindani wa muziki wa dansi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Alisema, wanatoa pole kwa familia yake, waandishi wa habari za michezo na wafanyakazi wenzake wote, wasanii na wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mdau mkubwa wa michezo na burudani.

Akimwelezea marehemu, Choki, alisema, Recho alikuwa mdau mkubwa wa bendi hiyo na alishiriki kuasisi Extra Bongo TP Sunday bonanza akishirikiana na baadhi ya waandishi wa habari za burudani kwa lengo la kuinua kiwango chao kimuziki hatua ambayo iliwaletea tija.

Alisema, Rachel, alishiriki kwa kiwango kikubwa kutoa ushauri wa kiufundi ndani na nje ya bendi na kutumia kalamu yake pia kuilezea vyema Extra Bongo hivyo ni vigumu kwa familia ya bendi hiyo kumsahau ambapo wanatarajia kuwasilisha rambirambi kwa familia ya marehemu kwa kushirikiana na Kamati ya mazishi.
mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA