Hatuko tayari kuingia doa la fedha za CHF-RC

   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dany Makanga akifungua mkutano wa wadau wa NHIF Mkoa wa Kigoma leo.

 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Gratian Mkoba akitoa salaam za Bodi kwa wadau.

  Mkurugenzi wa Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akiwa na mjumbe wa Bodi kumjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, John Mongela aliyelazwa kwa matibabu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akimjulia hali mwanachana wa Mfuko huo alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuona wanachama

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, Bwana Mongela akieleza namna alivyopatwa na homa kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF.
Mkurugenzi wa Raslimali watu wa NHIF, Beatus Chijumba akitoa elimu kwa mdau wa mfuko huo.



Na Grace Michael, Kigoma

UONGOZI wa Mkoa wa Kigoma, umesema hauko tayari kuona ukiingia doa la ufujaji wa fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) huku huduma za matibabu zikiendelea kudorola.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Dany Makanga katika mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao unajadili mambo mbalimbali ya namna ya kuboresha huduma za afya hususan kwa wanachama wake.

“Jamani hii aibu hatuko tayari kuendelea kuiona ni lazima fedha za wananchi zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa hasa ya kununulia dawa na vifaa tiba ili wawe na uhakika wa tiba sahihi,” alisema.

Kauli hiyo aliitoa baaba ya kubaini kuwa baadhi ya Halmashauri za wilaya mkoani humo hasa Wilaya ya Kibondo haina usimamizi bora wa fedha hizo na hata ufuatiliaji au uombaji wa fedha za tele kwa tele.

Kutokana na hali hiyo, aliagiza viongozi wote wa ngazi za halmashauri kujiwekea malengo ya uandikishaji wa kaya za kujiunga na CHF ili idadi kubwa iwe kwenye utaratibu wa bima za afya.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Gratian Mkoba, alisisitiza utumiaji wa fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo kwa kuwa ndiyo njia bora na pekee inayoweza kuboresha huduma za afya vituoni.

Katika hatua nyingine, uongozi wa NHIF ukiwa mkoani humo, umetoa jumla ya mashuka 1,140 katika vituo vilivyopo mkoani humo pamoja na kukutana na kikundi cha waendesha piki piki ambao walielimishwa namna ya kujiunga na CHF pamoja na faida zake kwa afya yao.

Akizungumza na kikundi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba alisema kuwa ni vyema wakaithamini kazi hiyo kwa kuwa ndiyo inawaingizia kipato na ili wawe na uhakika wa afya zao ni vyema wakajiunga na Mifuko ya Bima ya Afya ili wanapougua wawe na uhakika wa kupata matibabu.

NHIF katika ziara za kukutana na wadau mikoani, unatarajia kuhitimisha katika mikoa ya Rukwa na Dar es Salaam kati kati ya mwezi huu ambao utakuwa umefanikiwa kukutana na wadau nchi nzima na kuona hali ya vituo vya matibabu.

Cioo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI