ICD yazindua mtandao wa taarifa kuhusu walemavu



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu nchini Tanzania (ICD), Fredrick Mkatambo akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Kushoto ni Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii, Danford Makala aliyekuwa mgeni.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa ICD wakiwa katika hafla hiyo
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa ICD mara baada ya uzinduzi.
 
KITUO cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD) nchini Tanzania kimezindua mtandao (Blogu) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya walemavu na kuziweka katika mtandao huo ili wadau anuai waweze kujua taarifa hizo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo ambao utakuwa ukisimamiwa na ICD, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Fredrick Mkatambo amesema kwa muda mrefu imekuwa ni vigumu kupata taarifa zote juu ya masuala ya walemavu jambo ambalo ni moja ya vikwazo.
Alisema kuanzishwa kwa mtandao huo utasaidia wadau wa masuala ya walemavu ikiwemo Serikali kuingia na kupata taarifa mbalimbali zikiwemo changamoto inayokumbana nayo jamii hiyo na ikiwezekana wahusika kuwasaidia kundi hilo.
Aidha alisema “Najua kwa sasa kazi ni ngumu kupata taarifa muhimu juu ya masuala mbalimbali ya ulemavu…lakini naamini kwa sasa itakuwa ni rahisi maana tunasehemu ambayo unaweza kupata taarifa zote muhimu juu ya walemavu,” alisema Mkurugenzi.
Akifafanua namna mtandao huo utakavyokuwa ukifanya kazi, Mshauri wa Kiufundi kutoka kituo cha ICD, Natalia Lintner alisema katika blogu hiyo walemavu wanaweza kupata taarifa mbalimbali zinazowagusa kama ufadhili wa masomo, vyuo vikuu rafiki wa walemavu, matangazo muhimu yanayowagusa walemavu na habari za kawaida kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema taarifa nyingine ambazo zitakuwa zikioneshwa katika mtandao huo ni mashirika na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na watu wenye ulemavu na shughuli zake, pamoja na wadau anuai kuwa na uwezo wa kuchangia/kusaidia walemavu kupitia mtandao huo.
Naye Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii, Danford Makala akizindua mtandao huo pamoja na kitabu cha ‘Maisha Yangu’ ambacho kimeandaliwa na ICD na wafadhili wengine, alisema mtandao na kitabu hicho vitakuwa ni vyanzo vizuri vya taarifa kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema mtandao huo ambao ni sawa na jukaa la taarifa kuhusu watu wenye ulemavu litaisaidia Serikali pia kupata taarifa anuai juu ya masuala ya watu wenye ulemavu, ambazo zitakuwa chachu ya maboresho ya sera mbalimbali kila uchao.
“Hii ni njia ambayo watu wenye ulemavu wanaweza kupaza sauti yao kwa pamoja…kwa kutumia mtandao huu, tujitokeze kuchangia basi ili kweli mtandao huu uweze kufanya kazi ipasavya,” alisema Makala.
Kitabu cha maisha yangu ambacho kimezinduliwa pia katika hafla hiyo kimekusanya mahojiano ya watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam nia kuainisha changamoto mbalimbali katika maisha yao, hivyo kuleta picha halisi ya walemavu Tanzania.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)  

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA