KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI TUZO ZA MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA (TASWA)


 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Maounda akizungumza na waandishi wa habari kwenye klabu ya City Sports Lounge asubuhi hii wakati alipotangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando na katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto Kulia akitoa shukurani zake kwa kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamni tuzo hizo mwaka huu, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Nandi Mwiyombela Meneja miradi Endelevu SBL na Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL.
Kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza rasmi kudhamini kwa kitita cha shs 150M chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) katika tukio la kutoa tuzo kwa mwanamichezo bora wa mwaka.Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

 Tukio hilo la kihistoria litafanyika katika ukumbi maarufu hapa jijini Dar es Salaam Diamond Jubilee tarehe 14/06/2012 ambapo zaidi ya wageni 500 wanatarajiwa kufurika kushuhudia tukio hilo.

Akihutubia mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti bi. Teddy Mapunda, amesema maamuzi ya kudhamini tukio hilo kwa mara nyingine ni kuendelea kusaidia kuinua tasnia ya michezo hapa nchini. “Kufanya hivi ni sehemu mojawapo ya kuwatambua wanamichezo, lakini pia kupitia udhamini huu, tungependa kuwasaidia waandishi wa michezo kujaribu kuangalia ndani zaidi na kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii juu ya michezo mbalimbali iliyopo hasa hapa kwetu Tanzania”alisema Mapunda.

 Udhamini huu utatumika katika maeneo mbalimbali kufanikisha sherehe hiyo kama vile chakula cha jioni, burudani,tuzo, vyeti, zawadi pamoja na mahitaji na matumizi mengine ili zoezi hili liwe nzuri na la kukumbukwa nchini”, aliongeza Bi. Mapunda.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kuwa mdhamini mkuu wa tuzohizi kwa mwaka wa tatu sasa. “sisi kamaSBL kwakweli tunajivunia kuwa wadau wa tukio hili kwa mara nyingine, lakini pia tunajivunia kuwa na waandishi bora wahabari za michezo ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuinua na kuendeleza tasnia ya michezo hapa nchini kupitia taarifa sahihi zenye kuelimisha jamii juu ya swala zima la michezo” .

 Naye Mwenyekiti wa chama hicho TASWA Bw.Juma Pinto, ametoa shukrani zake kwa niaba ya TASWA kwa kampuni ya bia ya Serengeti na kusema kuwa wana faraja kubwa kwa kuona kampuni kama SBL inajitolea na kuwasaidia mwaka hadi mwaka kwa miaka mitatu sasa. Alisema kwamba wanatambua umuhimu wa kampuni hiyo(SBL) katika kusaidia kuinua michezo hapa nchini, “sisi hatuwezi kusema kitu,zaidi ya kushukuru sana kwa SBL kwakweli ni dhahiri kabisa  kuwa SBL inaendelea kubadilisha taswira ya michezo hapa nchini kwa mengi na haswa kwa kudhamini tukio hili la kutoa tuzo kwa waandishi bora wa michezo.Wamebadilisha tukio hili kuwa la kimataifa”, alisema Pinto.. Chanzo; Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA