KIKOSI IMARA CHA TAIFA STARS KUPATIKANA BAADA YA MECHI DHIDI YA MALAWI

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Kim Poulsen, amesema mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi ndiyo utakaompa sura ya kikosi chake kipya cha timu hiyo.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana mara baada ya mazoezi ya timu yake hiyo inayojiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan, alisema mechi dhidi ya Malawi ndiyo itakayompa kikosi chake.


Alisema kuwa ana amini kila mchezaji aliyemuita ana uwezo lakini ni nani watakuwa kwenye kikosi kitakachoivaa Ivory Coast hicho ndiyo kitapatikana mara baada ya mchezo huo.

"Ni kweli kila niliyemuhita nina amini anaweza lakini nani na niani watakakuwepo kwenye kikosi changu hicho nitajua mara baada ya mchezo wa wiki hii na Malawi.

Poulsen alisema wachezaji wake wana hali kubwa ya mazoezi na anaamini kil kitu kinawezekana katika mchezo wake ujao.

Stars itajitupa na timu ya Taifa ya Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kwenda mjini Abijan kuvaana na Ivory Coast 2 mwaka huu.

Wakati huo huo Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinawasili nchini leo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki.

Baadaye Malawi itakwenda Zanzibar kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zanzibar Heroes itakayofanyika Mei 28 mwaka huu kabla ya kuondoka Mei 30 mwaka huu kwenda Uganda ambapo Juni 2 mwaka huu itcheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.