MAFISANGO ALIJITABILIA KIFO

 Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba, marehemu Patrick Mafisango, tayari kutolewa heshima za mwisho jana kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.

KIPA wa timu ya Moro United, Jakson Chove amesema ni kama Patrick Mafisango alijitabiria kifo kutokana na mambo aliyofanya saa chache kabla ya kifo chake katika ukumbi wa Maisha Club uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam na kabla ya hapo.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwa mshambuliaji Emmanuel Okwi unapofanyika msiba wa Mafisango, kipa Chove alisema Mafisango ni rafiki yake mkubwa  ambaye walifahamiana tangu wakiwa Ruanda ambako walikuwa wakicheza soka wote.

Alisema ukiacha maisha ya soka, Mafisango kwake ni zaidi ya ndugu kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu na mara ya mwisho waliwasiliana muda mfupi kabla ya kupata ajali iliyochukua maisha yake.

"Nilizungumza na Mafisango akinitaka niende Maisha Club  nikaagane naye kabla ya kwenda kwao ambako ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Rwanda,"alisema Chove.

Alisema,"alinighasi sana mchana kutwa akitaka tuonane na alipoona simjali akaniambia niagizie chakula sehemu ambayo huwa tunakula na alinitumia fedha kwenye simu ili nilipe kabisa, nilifanya hivyo, lakini baada ya hapo niliondoka, ambapo Mafisango alipofika kula hakunikuta kitu kilichomfanya anitukane sana kwenye simu."

"Sielewi niseme nini kwa kuwa kifo hakikwepeki Mafisango alinibembeleza sana nionane naye jana, lakini nilikuwa mzito si ajabu ningekuwepo haya yasingetokea kwa kuwa mara nyingi akiwa amekunywa huwa namuendesha hadi kwake na baadaye napanda daladala narudi kwangu,"alisema Chove.

Akielezea jinsi alivyopata habari za msiba huo alisema baada ya kuona anamsumbua sana akimtaka aende Maisha Club ilibidi azime simu na alipoiwasha muda wa saa 10 na nusu alfajiri akapigiwa simu na mwanamuziki wa FM Academia aitwaye Hitler na kumuuliza kama amenusurika akiamini alikuwa naye.

"Nikashangaa nimenusurika nini ndio akaniambia kuwa Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari, sikuamini,  hata sasa siamini najilazimisha kuamini,"alisema Chove.

Aliendelea kusema kuwa Hitler alimpigia simu na kumwambia kuwa Mafisango ni kama kajitabiria kifo chake.

Akielezea kile alichokifanya Mafisango ukumbini hapo,  mwanamuziki Hitler wa kundi la FM Academia alisema Mafisango alikuwa amechangamka sana na mara nyingi alikuwa akipanda jukwaani kutunza fedha kama wafanyavyo 'mapedeshee'.

"Alinipa cheni ambayo alisema ina thamani kubwa na kuniambia ni kumbukumbu yangu nitamkumbuka sana nikiitazama cheni hiyo, sasa kwangu hayo ni mambo ya ajabu kwa Mafisango ingawa ni mpenzi wa bendi hii, lakini haya aliyofanya ni mapya kabisa,"alisema Hitler.

Chove aliendelea kusema kuwa alijuana na Mafisango tangu wapo Ruanda ambapo hata alipokuwa akitoka JKT kujiunga na Azam viongozi walimuuliza kuhusu mchezaji huyo kama anamjua na mazungumzo ya kwanza ya kujiunga na timu hiyo ni yeye ndio alifanya naye.

"Kabla ya kujiunga na Azam mimi ndio nilifanya mazungumzo naye kwanza kabla ya viongozi kwa kuwa waliniuliza uwezo wake kwani ndio nilikuwa natoka Rwanda hivyo nilikuwa namfahamu tangu huko,"alisema kwa uchungu Chove.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.