Mama Kikwete awataka wanawake kutokutoa mimba


Na Anna Nkinda – Maelezo, Mbeya
 Wanawake nchini wametakiwa kutokuwatupa watoto wanaowazaa hata kama wanakabiliwa na changamoto za kimaisha za kushindwa  kuwalea kwani kwa kufanya hivyo  wanamkosea Mwenyezi Mungu pia hawawezi jua watoto hao watakuwa na hali gani ya kimaisha kwa siku za baadaye.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake waliohudhuria  sherehe za  siku ya mwanamke wa Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo jijini Mbeya.
Aidha  Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  alisema  kuwa usawa wa kijinsia katika elimu na fursa za kiuchumi zimeendelea kuwa changamoto kwa  wanawake Duniani kote hata hivyo hatua kubwa imefikiwa ya  kuwakomboa wanawake wengi kutoka lindi la umasikini.
“Tunatambua kwamba wanawake wanaposhiriki kikamilifu katika shughuli za jamii uchumi wa nchi hukua zaidi. Hivyo siku kama ya leo ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wanawake kujifunza kutoka kwa wengine jinsi walivyofanikiwa , kubadilishana uzoefu na kuelimishana. Kwani elimu yenye manufaa ni ile inayolenga kuwakomboa watu kutokana na changamoto zinazowakabili”, alisema Mama Kikwete.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.