MEMBE ASEMA BADO HAJAOTESHWA URAIS

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hajaoteshwa kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Membe alisema harakati za kugombea urais siyo kitu kidogo cha kukurupuka, kwani unatakiwa kuwa na muono unaokujia kuwa mgombea.

“Usikurupuke tu, lazima uwe na kitu kinakutuma kuomba kugombea Urais, lakini sasa ninachosikia ni kutoka kwa watu kuwa nataka kugombea kitu ambacho hakina ukweli,” alisema Membe.
Membe alisema wakati alipotaka kugombea ubunge, alisikia sauti ikimtaka kugombea na akafanya hivyo, lakini kwa sasa bado sauti hiyo haijamjia.

“Sauti kama hii ilinijia wakati nilipotaka kugombea ubunge nami nilifanya hivyo, lakini sasa bado sauti hiyo haijanijia,” alisema Membe.

Katika hatua nyingine, Waziri Membe alielezea mkutano wa uchumi katika bara la Afrika ulioanza jana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, akisema unatokea katika kipindi cha uchumi katika bara hilo.
“Kwa mara ya kwanza unafanyika wakati bara la Ulaya zinaliangalia bara hili kwa kutafuta soko, ili kuwezesha nchi zao kuendelea,” alisema Membe na kuongeza:

“Hata ukiangalia dawa za kutibu malaria zinaletwa kwa wingi, lakini hakuna njia zinazofanyika ili kuuondoa ugonjwa huu na hii inafanyika ili kuviongezea viwanda vyao kuendelea.”
Membe alisema mkutano huo utatumika pia kujadili njia za kuhifadhi rasilimali zilizopo kwa bara hili, ili kuondoa kuwamilikisha watu wa dunia nyingine.

“Mpaka sasa ekari milioni 19 ya bara la Afrika zimeuzwa nje siyo mali yetu tena, zimekwishachukuliwa na watu wa Ulaya kitendo ambacho ni hatari,” alisema Membe na kuongeza:

"Mkutano huo pia utatafuta ufumbuzi wa tatizo la ajira hususan kuanzisha viwanda ambavyo vitaajiri wafanyakazi wengi na siyo kutengeneza viwanda, ambavyo havina manufaa yeyote kwa jamii."
Katika mkutano huo, Membe alisema mada inayojadiliwa mwaka huu ni Ukuaji wa Uchumi katika bara la Afrika na changamoto zake.

Membe alisema msimamo wa Serikali ya Tanzania ni kuunga mkono Sahara Magharibi kuwa nchi huru.
Membe alisema Tanzania inaamini sera ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya nchi hujitegemea na wananchi wake kuwa huru, hivyo harakati za kuwaunga zitaendelea.

“Kuna taarifa ambazo zinasambazwa kupitia mitandao ya jamii kuwa, Tanzania imejitoa hiyo naomba Watanzania watambue kuwa harakati hizo hazitakwisha hadi pale wananchi wa Sahara Magharibi watakapojitawala wao wenyewe,” alisema Membe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.