MJUE MISS EAST AFRICA 2012

 Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wanaendelea  kupatikana kutoka katika Nchi mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo.

Mrembo mwingine aliyeingia fainali ni Miss Lula Teklehaimanot (19) (pichani), kutoka Nchini Ethiopia ambae alipatikana mwishoni mwa wiki baada  ya kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Ethiopia katika fainali hizo.
 Miss Lula Teklehaimanot ana urefu wa 1.79m  na uzito wa 52kg ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha St. Merry University cha jijini Addis Ababa, Ethiopia ampapo anasomea Degree ya Marketing.

Pia Mrembo huyo ni miongoni mwa wanamitindo maarufu  wanaochipukia kwa kasi Nchini Ethiopia.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.Kwa hisani ya Daily Mitikas Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA