MUCCOBS MABINGWA POOL HIGHER LEARNING MKOA WA KILIMANJARO

 Wachezaji wa Chuo cha MUCCOBS wakipokea kitita cha Shilingi laki tano (500,000/=) mara baada ya kuibuka washindi wakati wa mashindano ya Pool Higher Learning yaliyomalizika mwishonimwa wiki Mkoani Kilimanjaro.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Shitungu na wa pili kulia ni Ofisa mauzo wa Mkoa wa Kilimanjaro, Edmundi Rutaraka.
 Ofisa mauzo wa Mkoa wa Klimanjaro, Edmundi Rutaraka (wapili kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha MUCCOBS zawadi ya ushindi wa kwanza Shilingi laki tano.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Shitungu
 Ofisa mauzo wa Mkoa wa Klimanjaro, Edmundi Rutaraka akizungumza na wanafunzi wa vyuo (hawapo pichani) wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Pool Higher Learning Mkoa wa Kilimanjaro
MASHINDANO ya Pool Higher Learning Mkoa wa Kilimanjaro Chuo cha MUCCOBS wameibuka mabingwa wa mchezo huo katika Mkoa wa Kilimanjaro hivyo kujinyakulia kitita cha Shilingi 500,000/=  baada ya kuwafunga chuo cha SMMUCO pointi 14-11wakati wa chezo wa fainali ulichezwa katika Klabu ya Makanyaga Kata ya Soweto Manispaa ya Moshi Mjini.
Washindi wa Pili katika Mashindani hayo ni SMMUCO ambao walizawadiwa kitita cha Shilingi 300,000/=,washindi wa tatu ni KCMUCO walipata 200,000/= na wane ni chuo cha MWUCE ambacho kilizawadiwa Shilingi 100,000/=
Upande wa Single wanaume(mmoja mmoja), Alphael  kutoka chuo cha MWUCE alitwaa ubingwa na kujitwalia 150,000/=akifuatiwa na Beatus Pius kutoka chuo cha MUCCOBS ambaye alishika nafasi ya pili na kujitwalia 100,000/= na Upande wa Singles wakinadada, Suche kutoka chuo cha MWUCE alitwaa ubingwa na kuzawadiwa 100,000/= na kufuatiwa na Maryviana kutoka Chuo cha MUCCOBS na kuzawadiwa 50,000/=
 Nahodha wa chuo cha SMMUCOBS akionyesha zawadi yao ya Shilingi laki tatu (300,000/=) baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo.
 Nahodha wa timu ya chuo cha KCMUCO akionyesha kitita cha shilingim laki mbili (200,000/=) baada ya kukamata nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo.
 Nahodha wa timu ya chuo cha MWUCE akionyesha kitita cha shilingim laki mbili (100,000/=) baada ya kukamata nafasi ya nne kwenye mashindano hayo
 Mshindi wa kwanza wa Singles wanaume, Alphael Jackson akionyesha kitita chake cha Shilingi laki moja na nusu (150,000/=) baada ya kukamata nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
 Mshindi wa kwanza wa Singles wanawake, Suche Atanasia kutoka chuo cha KCMUCO akionyesha kitita chake cha Shilingi laki moja na nusu (100,000/=) baada ya kukamata nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
 Mshindi wa Singles wanawake, Suche Atanasia  kutoka chuo cha KCMUCO akicheza
 Msindi wa pili Singles wanawake, Maryvianney Chizziel kutoka
chuo cha MUCCOBS

Wachezaji wa Chuo cha MUCCOBS wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI