MUME AMNYONGA MKEWE KWA WIVU

MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Esther Machia, (23) ameuawa kwa kunyongwa na mume wake, katika Kijiji cha Kazuni, wilayani Shinyanga.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku katika nyumba ya wanandoa hao.

Alisema mauaji hayo yametokana na wivu wa kimapenzi uliozaa ugomvi katika ya mume na mke katika siku ya tukio.Kamanda huyo alisema habari zilisema ugomvi huo ulitokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kuwa alikuwa na uhusiano na mtu mwingine nje ya ndoa.

Alisema katika ugomvi huo, mwanaume alimshambulia mkewe kwa kuchapa bakora katika sehemu mbalimbali za mwili wake na baadaye kumyonga shingo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, majirani walijaribu kumpeleka mwanamke huyo katika hospitali ya wilaya, ili kuokoa maisha yake lakini alifia njiani.“Uchunguzi wa awali wa madatari unaonyesha kuwa marehemu ilinyongwa shingi hadi akavunjika,” alisema Diwani.

Alisema tayari polisi wanamshikilia mtuhumiwa wa mauaji hayo na kwamba uchunguzi ukikamilika, atafikishwa mahakamani kujibu mashtaa ya mauaji.

Katika tukio lingine, watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia ambazo kama zingekuwa halali, zingekuwa na thamani ya Sh200,000.

Kamanda Diwani alisema watu hao walikamatwa juzi katika Kijiji cha Segese, wilayani Kahama.Alisema noti hizo zilikuwa zinapelekwa mnadani ambako zingetumika kununulia vitu mbalimbali

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA